Ask. Ngalalekumtwa: Haki na amani vitawale
ASKOFU wa Jimbo Katoliki Iringa, Mhashamu
Tarcisius Ngalalekumtwa ameongoza maelfu ya waamini wa jimbo hilo kufunga
kilele cha Mwaka wa Yubilei ya huruma ya Mungu huku akisisitiza kuwa haki na
amani havina budi kutawala kwa watu wote.
Askofu
Ngalalekumtwa amesema kwamba waamini wanaagizwa kuhurumia maudhi waliyotendewa
na wenzao na pia kushiriki shida za wenzo ziwe za kimwili au kiroho.
“Katekesi ya Kanisa Katoliki
inahamasisha kwamba kuwa na matendo ya huruma, mintaarafu mwili ni kama kulisha
wenye njaa, wenye kiu, kuwavisha wasio na nguo, kuwakaribisha wageni,
kutembelea wagonjwa,kuwaokoa waliotekwa na kuzikwa wakfu. Matendo ya kiroho ni
pamoja na kuwafunza wasiojua neno la Mungu, kuwashauri wenye mashaka, kuwaonya
wadhambi, kuvumilia mabaya” ameeleza
Maadhimisho
ya kufunga kwa mwaka wa huruma yalitanguliwa na maandamano yaliyohusisha
mapadri, watawa wa kike na kiume pamoja na waamini kutoka parokia 37 zilizopo
jimboni Iringa yakianzia katika Kanisa la Bikira Maria Consolta, Parokia ya
Mshindo, kupitia barabara ya Uhindini, Soko Kuu na baadae barabara ya Dodoma
hadi viwanja vya Kichangani Senta ya Vijana Parokia ya Kihesa.
Comments
Post a Comment