BORESHENI MAZINGIRA WANAYOISHI WAFUNGWA-PAPA FRANSISKO AWAASA VIONGOZI DUNIANI

VIONGOZI wa Jumuiya ya Kimataifa wametakiwa kuhakikisha wanaboresha maisha ya wafungwa magerezani ili kuwapa matumaini ya maisha japokuwa ni wakosefu. Hii itawasaidia kuwa raia wema pindi watakaporejea uraiani.

Haya ameyasema Papa Fransisko katika maadhimisho ya Jubilei ya wafungwa, ikiendana na Jubilei ya huruma ya Mungu inayoelekea ukingoni.

Papa Fransisko ameongeza kuwa ni vema pia suala la msamaha kwa wafungwa wanaostahili likapatiwa kipaumbele kwa kuzingatia haki na usawa.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU