“Ishini Kitakatifu”- Askofu Ruwa’ichi
WAKRISTO wameaswa kuchangamkia mambo ya kanisa zaidi na siyo ya
malimwengu ili waweze kuishi maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu na kuzingatia
utakatifu kama wito wa kila mbatizwa.
Wito
huo umetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi Katika homilia
yake kwenye adhimisho la ibada ya misa takatifu ya uzinduzi wa parokia ya NUNDU Jimboni humo.
Askofu
Rwai’chi katika ibada hiyo Ametoa “OLE” kwa wale wote wanao wakatisha wakristo
wengine tamaa wakati wanapojitahidi kufanya mambo matakatifu huku wakijiona
wapofu pamoja na kuwafananisha na watawa.
“Usimkatishe
tamaa mtu anayejitahidi kuishi maisha ya kimungu, mbona unafanya mambo
matakatifu sana kwani wewe ni mtawa?” Amesema Askofu Ruwai’chi.
Pamoja
na hayo Askofu Ruwa’ichi amesema wakristo wamekuwa na tabia ya kusifiana kwenye mambo madogo madogo hususani
ya kidunia badala ya kusifiana katika mambo ya kimungu, wakisahau ya kwamba wote ni wadhambi.
Akizungumzia
siku ya WATAKATIFU WOTE ambayo huazimishwa
kila mwaka tarehe mosi Novemba amesema kuazimisha siku hiyo ni tukio kubwa la
kikanisa ambalo wakristo wote ulimwenguni huwakumbuka waamini wenzao, wafuasi
wa Kristo ambao waliishi ukristo na utume wao kwa dhati bila ya kujibakiza na
hivyo baada ya ufuasi wao uliotukuka wakatukuzwa pamoja na Kristo.
“Nyerere
atatangazwa lini Mtakatifu?” hili ni swali ambalo Maaskofu wengi wa nchi za Afrika
wanapenda kuniuliza pindi ninapokutana nao kwenye mikutano.
Huu ni
mfano mzuri kwa nchi ya Tanzania kwani swali kama hilo linaonyesha dhahiri
kwamba mchango wake katika jamii ulionekana hivyo ni vema sana kwa wakristo
wote kufanya mambo mengi yatakayowafanya watu wawe na sababu za kuwaona
watakatifu na endapo watu hawatayaona utakayokuwa ukiyaishi mwishowe utavikwa taji
mbinguni”.
Comments
Post a Comment