HURUMA YA MUNGU HAINA MIPAKA





KATIBU mkuu wa Jimbo Katoliki Morogoro Padri Luitfrid Makseyo ametoa wito kwa waamini kutambua kuwa huruma ya Mungu haina mipaka hivyo ni wajibu wao kuitafuta huruma hiyo.

Padri Makseyo amesema hayo hivi karibuni ofisini kwake alipotembelewa na gazeti hili katika mazungumzo maalumu akieleza baadhi ya mikakati ya Jimbo katika hitimisho la mwaka wa Jubilei ya huruma ya Mungu.

Amesema hitimisho la kufunga rasmi Jubilei ya huruma ya Mungu isiwe sababu mojawapo ya waamini kuacha matendo ya huruma katika nyanja mbalimbali za maisha ya kiroho.

“kufunga rasmi jubilei hii ya Mwaka Wa Huruma ya Mungu isiwe chanzo cha waamini kuacha kutenda mema, niwaombe muendelee kutenda mema ya huruma katika nyanja mbalimbali za maisha ya kiroho na kwa jamii zinazotuzunguka,” amesema Padri Makseyo.

Kuhusu migogoro mbalimbali inayowakabili baadhi ya wanandoa hatimaye kutengana, amewashauri wenye vikwazo hivyo kuutumia vyema mwaka huu wa huruma ya Mungu kumaliza mikwaruzano yao ili waweze kushiriki sakramenti mbalimbali za kanisa.

“wanandoa wenye migogoro tumieni mwaka huu wa huruma ya Mungu kutatua migogoro inayowakabili ili muweze kushiriki sakramenti mbalimbali za kanisa,” amesema Padri Makseyo.

Maadhimisho ya mwaka mtakatifu wa huruma ya Mungu kwa Jimbo la Morogoro yatafungwa rasmi Novemba 19 mwaka huu kwa kufanya hija takatifu itakayoanzia katika kanisa kuu la Mtakatifu Patris hadi kanisa la Mwili na damu ya Yesu kola.

Mwaka mtakatifu wa Huruma ya Mungu ulizinduliwa rasmi na Baba Mtakatifu Fransisko Desemba 8, 2015 na kitaifa utahitimishwa mwishoni mwa mwaka 2016.

Na Josephine Burton, Morogoro.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU