Ask. Shao: Lazima tujifunze kusamehe
WAKRISTO nchini
wametakiwa kuwa na huruma na kujifunza kusamehe ili kuendeleza
amani na upendo uliopo baina yao na waamini wa dini nyingine.
Hayo yameelezwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Zanzibar Mhashamu
Augustino Shao wakati akifunga maadhimisho ya Mwaka wa Yubilei ya Huruma
Ya Mungu visiwani Zanzibar
Amesema kuwa ni vyema wakristo wakawa na huruma bila ya
kuweka malipizi au visasi kutokana na mambo mengi yaliyotokea ikiwemo
kuuawa mapadri huku wengine wakijeruhiwa.
Hata hivyo Askofu Shao amesema kuwa wakristo wasamehe
kwa moyo wa upendo bila ya kuweka kinyongo chochote katika nafsi zao ili
kudumisha amani, upendo na utulivu katika visiwa vya Zanzibar.
Pia amebainisha kuwa upendo na utulivu ni njia
mojawapo ya kudumisha amani nchini na ya kuleta maendeleo hivyo
hakuna budi kuienzi na kuitunza.
Wakati huohuo Askofu Agustino
Shao ametoa mafunzo kuhusu mafuta ya upako wa wagonjwa kwa kubainisha kuwa
mafuta hayo si ya wagonjwa tu bali ni kwa wakristo wenye kubatizwa na
wenye ndoa ya kikristo.
Comments
Post a Comment