"VIROBA MARUFUKU" WAZIRI MKUU
SERIKALI
imeziagiza kampuni zote zinazozalisha vinywaji vya pombe kali zenye
vibali vyote kubadilisha teknolojia ya ufungaji wake na kuweka vinywaji hivyo
kwenye chupa kutoka katika vifungashio vidogo(maarufu viroba) .
Agizo
hilo limetolewa mjini hapa hivi karibuni na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati
akifungua kikao cha baraza la mawaziri ambacho ni cha kwanza kufanyika mkoani
Dodoma baada ya serikali kuhamia Dodoma.
Hata
hivyo Majaliwa ameeleza namna ambavyo Tume ya kuratibu uthibiti wa dawa
za kulevya nchini inavyoendelea na utendaji wake wa kazi ambapo imekamata na
kuwatia hatiani watuhumiwa 76 waliokutwa dawa za Viwandani, ambazo ni Heroine
na Cocaine.
Moja
ya ajenda katika kikao hicho ilikuwa ni mawaziri ambao ni wajumbe wa Tume
hiyo kupokea taarifa ya kazi iliyokwisha fanywa na katika kukabiliana na
kukamata kwa dawa za kulevya tangu kuanza kazi kwa tume hiyo.
Ajenda
nyingine ni wizara kutoa taarifa na idadi ya watumishi
waliohamia Dodoma kwa awamu ya kwanza kati ya watumishi wangapi waliopo kwenye
Wizara na kueleza wanadhani Wizara zao kwa mpango waliojiwekea watakamilisha
lini kuhamia Dodoma na katika awamu ngapi kati ya awamu sita zilizopangwa.
Mbali
na hayo ameitaja nyingine kuwa ni kupokea taarifa ya matumizi ya fedha na
miradi ya maendeleo kwa mwezi julai 2016 hadi februari 2017 agenda, ajenda
mbayo haitajadiliwa kama mwanzo kwa kila wizara kutoa taarifa ya fedha iliyoingia
na kazi zilizofanywa na badala yake watapata taarifa kutoka kwa Waziri wa fedha
na kila wizara itakwenda kufanya mapitio na kujiweka vizuri.
Wakati
huo huo waziri mkuu ametoa taarifa ya mwenendo wa vita ya dawa za kulevya
nchini,ambapo alisema Tume hiyo ilianza kazi Februari mwaka jana, na
katika kipindi cha Julai 2016 hadi Januari 2017 jumla ya watuhumiwa 11503
wamekamatwa kwa kujihusisha na uzalushaji, uuzaji uzambazaji na utumiaji wa
dawa hizo.
Majaliwa,
amebainisha kuwa, kati ya watuhumiwa hao 11503, watuhumiwa 981i walikutwa
na kesi za kujibu huku 974 wakitiwa hatiani baada ya kubaini kuhusika na
makosa hayo.
Katika
kikao hicho waziri mkuu amewaagiza mawaziri wote ambao ni wajumbe wa baraza la
tume ya kuratibu udhibiti wa dawa ya kulevya nchini kushiriki kikamilifu katika
vita hiyo huku akiwakabidhi namba ya kamishina wa dawa za kulevya ili waweze
kumpatia taarifa mara wanapokutana na matukio yanayohusiana na dawa za kulevya.
“Taarifa
hii imehusisha dawa za viwandani pekee bila kuhusisha bangi na mirungi huku
akipongeza mapambano yanayofanywa katika mikoa yote juu ya vita hiyo pamoja na
kuwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mamlaka zote zinazohusika
bila woga,”amesema.
Kuhusu
pombe haramu na pombe zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki maarufu
kama viroba waziri mkuu amesema, msako wa kuondoa bidhaa hizo ambazo zilikuwa
zikihatarisha ustawi wa taifa unaendelea.
Amesema
katika msako huo walibaini kuwepo kwa kwa makampuni yanayozalisha pombe hizo
bila vibali huku wengine wakiweka pombe haramu ya gongo kwenye viroba hivyo.
Katika
hatua nyingine waziri mkuu amezungumzia kukamilika kwa mawaziri wote kuhamia
Dodoma huku akiwataka kufanyia shughuli zao zote mkoani humo.
Vile
vile amesema, awali waliweka utaratibu wa kuhamia Dodoma kwa awamu ambapo
zipo awamu sita na awamu ya kwanza ilikuwa inaanza Agosti 2016 hadi februari
mwaka huu ambao ilihusisha mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi na wote
wanaofanya kazi kwa pamoja.
Na
Dotto Kwilasa,Dodoma.
Comments
Post a Comment