SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..
SALA YA ASUBUHI.
Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Ee Baba yetu Mungu mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba, Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi, nikutii.
Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.
Mlinzi mkuu malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwako juu. Amina.
NIA NJEMA.
Kumheshimu Mungu wangu
Namtolea roho yangu,
Nifanye kazi nipumzike
Amri zake tu nishike
Wazo, neno, tendo lote
Namtolea Mungu pote
Roho, mwili chote changu,
Pendo na uzima wangu
Mungu wangu nitampenda,
Wala dhambi sitatenda.
Jina lako nasifia,
Utakalo hutimia.
Kwa utii navumilia
Teso na matata pia.
Nipe, Bwana, neema zako
Niongeze sifa yako. Amina.
SALA YA MATOLEO.
Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu Baba mwenyezi. Muumba wa Mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristo Mwanae wa pekee, Bwana wetu. Aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria. Akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato. Akasulibiwa, akafa, akazikwa; akashukia kuzimu. Siku ya tatu akafufuka katika wafu. Akapaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi. Toka huko atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele ijayo. Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu Miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria misa takatifu, dominika na sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya jumatano ya majivu; usile nyama siku ya ijumaa kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi takatifu hasa wakati wa Paska.
5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.
SALA YA IMANI.
Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.
SALA YA MATUMAINI.
Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.
SALA YA MAPENDO.
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu. Kwani ndiwe mwema, ndiwe nwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako, nipate kurudi. Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI.
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina.
MALAIKA WA BWANA
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Salamu, Maria,.....
Ndimi mtumishi wa Bwana.
Nitendewe ulivyonena.
Salamu, Maria....
Neno la Mungu akatwaa mwili.
Akakaa kwetu.
Salamu, Maria....
Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.
Tujaliwe ahadi za Kristu.
Tuombe
Tunakuomba, Ee Bwana, utie neema yako mioyon mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. AMINA..
ATUKUZWE (mara tatu)
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Asante Mungu atujarie kutambuwa uwepo wake mara baada ya kuamka, ni jambo jema kumshukuru na kumuomba kwani yeye ndiye msaada peke yake kwa binadamu wote. Roho mtakatifu wa bwana atuongoze katikati maisha yetu siku zote tutamshinda shetani.
ReplyDeleteAminaa 🙏
DeleteAmina
DeleteMungu twaomba usikie maombi yetu
DeleteEe Mwenyezi Mungu pokea maombi yetu🙏
DeleteAmina
DeleteAmen
DeleteAmina
DeleteAmina,
DeleteNawatakia asubuhi njema wapendwa
Amina
DeleteAmen
DeleteAsante mungu kwa neema unazotujalia!
ReplyDeleteAmeen 🙏
DeleteAmina
DeleteMungu akubariki sana
ReplyDeleteMungu wetu
ReplyDeleteMungu awe nawe pamoja daima.
ReplyDeleteAsante kwa msaada mkuu.. Mungu awe nasi
ReplyDeleteAsanteni mbarikiwe
ReplyDeleteAmina
DeleteAMINA
ReplyDeleteMwenyez Mungu Awabariki
ReplyDeleteEmwenyezi Mungutunakuomba baraka tunaomba kibali katika kazi zetu tunawaombea pia wazazi wetu viongozi wetu wa dini na waserikaki roho mtakatifu akatende pamoja nao naomba hayoyote kwa njia ya kristu bwana wetu amina
ReplyDeleteMungu ni mkuu sana,ni vyema kumshukuru kila tuamkapo
ReplyDeleteAsante Mungu kwa neema ulizotujalia
ReplyDeleteTusisite katika sala!
ReplyDeleteAsante Mungu
ReplyDeleteSali kila wakati
ReplyDeleteTusali maana hatujui siku wala SAA,eemwezi mungu tujalie tuwe watiifu.
ReplyDeleteAmina
ReplyDeleteAmina
ReplyDeleteAmina! Amina! Amina!
ReplyDeleteAmina nashukuru sana kwa kupata huduma hii nzuri ya kiroho Mungu aendelee kutujaalia kila lililo jema tukabarikiwe sote, Amina
ReplyDeleteAmina
ReplyDeleteAMEN
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteNi vyema wapendwa kuamka na sala hii inatupa afya kiroho
ReplyDeleteMungu Baba, tunakushukuru kwa yote unayotujalia, tunakushukuru kwa amani tuliyonayo Watanzania.
ReplyDeleteTunakushukuru Bwana umeiumba Dunia iwe sehemu ya amani na umetupa maarifa ya kuweza kushi vema. Lakini Baba ubinafsi, upofu na ukiziwi wa wenye macho na masikio umeumpa Binadamu kiburi na majivuno na hivi vimeleta mifarakano, vita, magonjwa na hofu, njaa, ukimbizi na tabu kwa baadhi ya watu wako wasiokuwa na hatia!
Tunakuomba Baba
1.Umdhoofishe kila mwenye nia hovu anayesababisha usumbufu kwa watu wako walioko: Ukraine_ Afghanistan, Mashariki ya Kati na kwingineko kote duniani. Ehe Baba usituache watu wako tukateseka. Kwani Bwana tunaamini mamlaka zote zitawalazo zimetoka kwako.
NA HIVYO BABA
2.Umuondolee Kibali cha uongozi kiongozi yeyote muovu anayevunja amani ya Dunia kwa sababu yoyote iwayo.
3.Uwarejeshee furaha wote wanaosononeka kwa mateso ya udhalimu wowote ule
4.Uwape hekima ya kutambua nia ya uumbaji wako wa Binadamu na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana hapa duniani
5. Kwa rehema yako Ehe. Bwana utujalie kuyashika mafundisho yako na kuyaishi
Amina
Amen
DeleteAmeen
DeleteEEH BWANA MUNGU WANGU, NAOKUOMBA UNIZIDISHIE HEKIMA, AKILI NA BUSARA. VITAKAVYONIWEZESHA KUPATA UFANISI KATIKA SHUGHULI ZANGU ZOTE, KIELIMU, KIBIASHARA NA KIKILIMO. UNIONGOZE VYEMA KATIKA NDOTO ZA MALENGO YANGU ILI NIEWEZE KUFIKA KILELE CHA MAFANIKIO HAPA DUNIANI NA MBINGUNI. AMINA.
ReplyDeleteEwe mwenyezi MUNGU nasadiki kwako ulimfufua Yesu naomba unirehemu mimi mwenye dhambi. Amen
ReplyDeleteAsante kwa sala hii Mungu Awabariki sana
ReplyDeleteSteven Lazaro
DeleteAHSANTE MUNGU KWA NEEMA UNAZOTUJALIA
ReplyDeleteAsante mungu kwa kupata baraka hizi
ReplyDeleteAnsate Mungu
ReplyDeleteMungu baba ninakushukuru Sana kwa loho wako mtakatifu kunikumbusha nikushukulu asbh ya leo amina.
ReplyDeleteAsante Mungu kwa Neema na Baraka kwa kunijalia Afyya njema.si mwema sana mbele zako bari ni huruma yako na upendo kwangu.Sida na utukufu ni vyako milele na milele Amina.
ReplyDelete🙏
DeleteAmina
ReplyDeleteKwenye sala ya Malaika wa Bwana ipi ni sahihi " ... tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko..." au "tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko"?
ReplyDeleteMungu Ni Wetu Sote 🙏🏾
ReplyDeleteNi kwenye utukufu wa ufufuko
ReplyDeleteAmina
ReplyDeleteAmina
ReplyDeleteAmina, Tumsifu Yesu kristo...
ReplyDeleteAminaa bariki na Kaz zetu
ReplyDeleteGreat and that i have a dandy offer: What Home Renovation Shows Are On Netflix complete home remodeling
ReplyDeleteAmina Tumsifu Yesu Kristu
ReplyDeleteAsante yesu kwa wema wako maishani mwangu
ReplyDelete