BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI LAADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI,SIKUKUU YAFANA SANA KATIKA PICHA HIZI
























Baraza la maaskofu katoliki nchini Tanzania TEC hapo jana limeadhimisha sikukuu ya wafanyakazi tukio lililofanyika huko Bagamoyo huku katibu mkuu wa baraza hilo Padri Raymond Saba akiwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa umakini,weledi,malengo,upendo,kusaidiana,misimamo huku wakimtanguliza Mwenyezi Mungu.

Kabla ya burudani mbalimbali kufanyika katika sikukuu hiyo,misa maalum ilifanyika kuliombea baraza,taifa,wafanyakazi,kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki,wagonjwa na watu waliotoa mchango katika baraza.

Michezo kadhaa ilifanyika mbali na chakula na vinywaji vya kutosha,michezo iliyofanyika ni kucheza muziki,kuogelea,kuvuta kamba,kukimbia,kuimba,kucheza mpira nakadhalika.

Washiriki wote walilidhika na sikukuu hiyo huku wakiomba mwakani wapate fursa ya kufanya tukio hilo huko Ngorongoro.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU