Posts

Showing posts from 2017

MAGAZETINI LEO JUMATANO DEC 20, 2017

Image

Papa Francisko kutembelea S. Giovanni Rotondo 17 Machi 2018

Image
Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 tangu alipofariki dunia Mtakatifu Padre Pio wa Pietrelcina, tarehe 17 Machi 2018 anatarajiwa kufanya hija ya kichungaji mjini Pietrelcina, Jimbo Katoliki la Benevento, Italia. Maadhimisho haya yanakwenda sanjari na Jubilei ya Miaka 50 tangu Madonda Matakatifu yalipojitokeza kwenye mwili wa Padre Pio alipokuwa katika huduma huko San Giovanni Rotondo, Jimbo Katoliki la Manfredonia-Vieste. Haya yamebainishwa na Dr. Greg Burke, Msemaji mkuu wa Vatican, Jumanne, tarehe 19 Desemba 2017 Itakumbukwa kwamba, Mtakatifu Padre Pio alizaliwa kunako tarehe 25 Mei 1887 huko Pietrelcina, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi na Kitawa, alipadrishwa kunako tarehe 10 Agosti 1910 na kufariki dunia kunako tarehe 23 Septemba 1968 huko San Giovanni Rotondo. Alitangazwa kuwa Mtakatifu na Papa Yohane Paulo II kunako tarehe 16 Juni 2002 na Mama Kanisa anafanya kumbu kumbu yake kila mwaka ifikapo tarehe 23 Septemba.

TUJIFUNZE MFANO WA MTAKATIFU YOSEFU KATIKA KUVUMILIA MATATIZO NA GIZA!

Image
Katika matatizo, huzuni na giza, tujifunze kutokana na Mtakatifu Yosefu ambaye anatambua namna ya kutembea gizani, anavyosikiliza sauti ya Mungu na kama anavyokwenda mbele kwa ukimya.  Huo ndiyo ushauri wa Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumatatu 18 Desemba 2017 katika mahubiri yake kwenye Kanisa cha Mtakatifu Martha mjini Vatican. Ametafakari hayo akitazama Injili ya siku ya Mtakatifu Matayo, ambayo inaeleza kuwa, juu ya uzao yaani, Yesu atazaliwa na Maria mchumba wa Yosefu mwana wa Daudi. Baba Mtakatifu akitafakari zaidi anaonesha mshituko wa Yoseph, hasa Maria alipoanza kuwa na ishara za kuonesha ujauzito na zaidi mara baada ya Maria kurudi kutoka kwa Elizabeth. Ni wazi kuonesha wasiwasi wa mtu huyo katika uchungu na mateso kwa maana watu katika kijiji kile walianza maneno. Na kwa upande wa Yosefu hakuwa na ulewa kama Maria alikuwa mama wa Mungu na ndiyo maana aliamua kumwacha kwa kimya bila kumtangaza kwa umma, hadi Bwana alipoingilia kati kwa njia ya malaika katika ndoto a

MAGAZETINI LEO JUMANNE DES 19

Image

Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumatatu ya Disemba 18

Image