TUJIFUNZE MFANO WA MTAKATIFU YOSEFU KATIKA KUVUMILIA MATATIZO NA GIZA!

Katika matatizo, huzuni na giza, tujifunze kutokana na Mtakatifu Yosefu ambaye anatambua namna ya kutembea gizani, anavyosikiliza sauti ya Mungu na kama anavyokwenda mbele kwa ukimya.  Huo ndiyo ushauri wa Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumatatu 18 Desemba 2017 katika mahubiri yake kwenye Kanisa cha Mtakatifu Martha mjini Vatican. Ametafakari hayo akitazama Injili ya siku ya Mtakatifu Matayo, ambayo inaeleza kuwa, juu ya uzao yaani, Yesu atazaliwa na Maria mchumba wa Yosefu mwana wa Daudi.

Baba Mtakatifu akitafakari zaidi anaonesha mshituko wa Yoseph, hasa Maria alipoanza kuwa na ishara za kuonesha ujauzito na zaidi mara baada ya Maria kurudi kutoka kwa Elizabeth. Ni wazi kuonesha wasiwasi wa mtu huyo katika uchungu na mateso kwa maana watu katika kijiji kile walianza maneno. Na kwa upande wa Yosefu hakuwa na ulewa kama Maria alikuwa mama wa Mungu na ndiyo maana aliamua kumwacha kwa kimya bila kumtangaza kwa umma, hadi Bwana alipoingilia kati kwa njia ya malaika katika ndoto ambaye alimweleza kuwa mtoto atakayezaliwa naye ni kwa njia ya Roho Mtakatifu na kwa njia hiyo Yoseph aliamini na kutii.

Yoseph alipata mapambano ya ndani ya roho yake, mapambano hayo yalikuwa na sauti ya Mungu, japokuwa sauti ile mara nyingi ilikuwa ni mwanzo wa utume wake, kama isikikavyo mara kwa mara katika Biblia, na ndiyo sauti ile ya “amka na umchukue Maria nyumbani mwako”.
Ilikuwa ni kumwakikishia juu ya wajibu wake katika hali hiyo; hali ambayo alitakiwa   kuwa nayo mikononi mwake na kwenda mbele. Lakini Baba Mtakatifu anafafanua kwamba Yosefu hakwenda kwa marafiki kutafuta ushauri, hakwenda wa wataalam ili watafsri ndoto yake, yeye aliamini tu na kuendelea mbele.

Alichukua wajibu huo mikononi mwake. Lakini ni kitu gani alitakiwa kuchukua mikononi mwake Yesefu? Hali yake ilikuwaje? Je Yosefu alikuwa abeba nini? Baba Mtakatifu ametoa jibu kwa, Yosefu alitakiwa kuwajibika kwa mambo mawili: kwanza ubaba na ile ya fumbo! Nini maana ya kubeba ubaba: Anaongeza kusema, yeye alitakiwa kubeba ubaba. Kwa maana ni kitu kilichotambulika tayari kwenye uzao wa Yesu ambapo kama wanavyoeleza kwamba alikuwa ni mwana ya Yoseph. Yeye alibeba mzigo, huo wa ubaba ambao haukuwa wake: kwa maana ulitokana na Baba. Yeye alipeleka mbele ubaba ukiwa na maana ya kwamba si katika kusaidia Maria na mtoto, bali hata kufanya mtoto akuwe , kumfundisha kazi, hadi kumfikisha katika ukomavu wa kiume. Yosefu alichukua jukumu la ubaba usiyo wa kwake, bali wa kutoka kwa Mungu na alibeba bila kusema neno lolote.

Katika Injili zote hawasemi neno lolote lililotamkwa na Yosefu. Ni mwanaume kimya na   mtiifu wa ukimya. Yeye alichukua fumbo mikononi mwake ili kuwapeleka watu wa Mungu, kama inavyoeleza katika somo la kwanza kwamba, ni fumbo la kuwapeleka kwa Mungu, ni fumbo la uumbaji ambalo liturujia inaonesha maajabu ya kazi ya uumbaji. Na ndiyo maana Yosefu alichukua mikononi kwake fumbo hili na kusaidia kwa ukimya wake, katika kazi yake hadi ilipotimia wakati wa kuitwa kwake na Mungu.

Mwanaume huyo Baba Mtakatifu anabaisha, alibeba ubaba na fumbo, ambalo lilitwa kivuli cha Mungu Baba. Na iwapo Yesu alijifunza kuita baba kwa baba yake, aliyekuwa anamfahamu kama Mungu, ilitokana na kujifunza maisha kutokana na ushuhuda wa Yosefu mwanaume ambaye alimlinda, mwanaume aliye mfanya akue na mwanaume anayepeleka maana na kila fumbo lakini bila kuwa na lolote la kwake. Baba Mtakatifu amemalizia kwa kusema, Yosefu ni mtu mkubwa ambaye Mungu alikuwa na haja naye ili aweze kupeleka fumbo la kuwarudisha watu wake kuelekea katika uumbaji mpya.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI