Posts

Showing posts from February, 2018

Jumuiya ya Kimataifa ishikamane ili kupambana na changamoto mamboleo

Image
Tunawezaje sasa kujenga maisha ya siku za usoni yenye kukirimiana na kushirikishana, iwapo dunia inaonekana kushamiri kwenye mipasuko na kinzani? Tunawezaje leo kulisha wanyonge na kusimamia wokovu kutoka kwenye baa la njaa, iwapo dunia inayoonekana leo kuwa kama kijiji kufuatia maendeleo ya utandawazi, ndiyo dunia hiyo hiyo inayojidhihirisha kwa mmong’onyoko wa maadili na tunu njema. Maswali haya yanarushwa na Dr. Olav Fykse Tveit, Katibu mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, katika kuhitimisha Jukwaa la Uchumi na Biashara duniani,  Wolrd Economic Forum , lililofanyika hivi karibuni huko Davos, nchini Uswiss, tarehe 22 – 26 Januari 2018. Maswali haya yamekuwa kama mwiba kwenye miili na mioyo ya washiriki wengi katika Jukwaa hilo, ambalo lilihudhuriwa na viongozi na watendaji wengi wa serikali, siasa, fedha na uchumi, jamii, usalama na dini kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni. Jukwaa hilo limefanyika wakati muafaka, anasema Dr. Olav Fykse Tveit, wakati ambapo dunia inaonekana k

TAIFA LINAKOSA DIRA KWASABABU YA KUZIKA AZIMIO LA ARUSHA- ASKOFU NYAISONGA

Image
Na Sarah Pelaji, Dar es Salaam. BAADA ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kutoa Ujumbe wa Kwaresima kwa mwaka 2018 unaobebwa na kauli mbiu “Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu” (Mt. 28:19), Askofu wa Jimbo Katoliki Mpanda Mhashamu Gervas Nyaisonga amesema kuwa, ujumbe huo umeandikwa kulingana na nyakati za sasa ambapo taifa linahitaji kurejea Azimio la Arusha ili kuleta ustawi wa watu wote bila ubaguzi na bila kuchochea matabaka. “Ujumbe huo umeandikwa ili kutafakari kwa kina mambo makubwa matatu: Kwanza, Mwaka huu wa Jubilei ya miaka 150 ya uinjilishaji Tanzania (1868-2018). Pili, Mwaka wa 50 tangu Kanisa la Tanzania lilipounga mkono siasa ya Azimio la Arusha zilizosisitiza udugu , kumegeana , kuhudumiana na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Kanisa liliona azimio la Arusha lilikuwa linadai kudhihirisha imani kwa matendo (Yak. 2: 14-17). Tatu, Kuhamasisha maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa mwaka 2019,” amesema Askofu

JUMAPILI YA 4 YA KWARESIMA SIKU YA KUCHANGIA JUBILEI YA MIAKA 150 YA UINJILISHAJI

Image
Na Sarah Pelaji, Dar es Salaam w AKATI Kanisa Katoliki nchini linajiandaa kushurehekea Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara,  Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetangaza kuwa, Dominika ya 4 ya Kwaresima mwaka huu, yaani  11 Machi 2018, sadaka zote za Misa Takatifu za siku hiyo kwa nchi nzima (vigango, parokia, Majimbo yote Tz) zitakusanywa na kuwasilishwa TEC ili kusaidia maandalizi ya maadhimisho ya Jubilei hiyo. Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Euzebius Nzigilwa amesema kuwa hayo ni maazimiao ya   Mkutano wa TEC wa Januari 25 mwaka huu . Kauli mbiu ya Jubilei hiyo ni ‘Miaka 150 ya Uinjilishaji, Furaha ya Injili.’ “Machi 11 mwaka huu yaani Jumapili ya 4 ya kwaresima (Laetare) hakutakuwa na michango mingine yoyote ya kiparokia siku hiyo. Sadaka yote ya kwanza na ya pili ikusanywe na kupelekwa Jimboni ili iweze kuwasilishwa Taifani. Pia jumapili hiyo itumike kwa ajili ya kuhamasisha   waamini juu ya maadhimisho ya