WAKATOLIKI WAASWA KUJITATHMINI KIPINDI CHA KWARESMA
n Na Agnes Shayo, Dar es Salaam
Waamini
Wakatoliki nchini, wameaswa kujitafakari na kujitathmini ndani ya nafsi zao,
kuhusiana na safari ya siku 40 za kipindi cha Kwaresma kisha kila mmoja kuona
kwamba anahitaji huruma ya Mungu, ikiwa ni pamoja na kufanya mapinduzi ya
Kiroho.
Wito huo umetolewa na Padri Francis Mtema, ambaye ni Makamu
wa Askofu namba mbili wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza wakati akitoa homilia yake
kwa waamini wa Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Jimbo Kuu Katoliki
Mwanza wakati wa adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu ya Jumatano ya Majivu.
Padri Mtema amesema kuwa amewakumbusha waamini kuwa kufunga
si chakula tu, bali amewataka watambue kuwa vipo vitu mbalimbali vya kufunga
katika kipindi hiki cha Kwaresma, ikiwa ni pamoja na yale yote yanayomuweka
mkristo mbali na muumba wake, kama vile kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya
kijamii, kwenye starehe, kutotimiza wajibu kazini, nyumbani au katika familia
nk.
Wakati huo huo, Paroko wa Parokia ya Mikocheni Padri Adrea
Mwekibindu, amezungumzia kuhusu kupakwa Majivu, akisisitiza kuwa, hii ni ishara
ya kutakaswa/kusafishwa na ubaya wote wa dhambi ili kufanywa upya na
kumrudia Mungu, huku akiwasihi kila mmoja kushiriki toba hii katika kipindi
hiki cha Kwaresma, pasipo kujali umri rangi wala muonekano, maana huruma ya
Mungu iko wazi hivyo kila mmoja anaalikwa kuikimbilia.
Aidha amewakumbusha kuziishi nguzo kuu tatu ambazo ni muhimu
kwa kila mmoja kuzifuata, huku akisema kuwa Mosi ni Sala, na kuwasaida
wahitaji.
Kuhusu kufunga Padri Mwekibindu amesema kuwa kunawahusu wote
wenye nguvu ili kuitisha miili yao, huku akiwataka kuwagawia wahitaji yale
ambayo watakuwa wamejinyima wakati wote wa kwaresma.
Safari ya Kwaresma imeanza siku ya Jumatano ya majivu na
Itadumu kwa siku 40, ambapo Baraza la maaskofu limetoa ujumbe wenye Kauli Mbiu
inayosema “Basi enendeni mkawafundishe mataifa yote kuwa wanafunzi wangi.
Comments
Post a Comment