WAHASIBU NA WASIMAMIZI WA MIRADI YA MAJIMBO KATOLIKI WAFUNDWA
Matukio
mbalimbali yanayojiri katika ufunguzi wa semina inayowakutanisha wahasibu na
wasimamizi wa miradi wa majimbo katoliki mbalimbali nchini, inayofanyika katika
Kituo cha Kurasini-Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Semina hiyo
inayolenga kuwajengea uwezo wa usimamizi wa fedha na miradi washiriki hao
imeandaliwa na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki
(AMECEA) kwa kushirikiana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
“Kama Kanisa
tunapaswa kuwa mstari wa mbele kufuata sheria za kodi za nchi. Sheria na
taratibu hizi siyo ngeni, zilikuwepo katika nchi yetu ila zilikuwa hazisimamiwi
vizuri na kufuatiliwa” Katibu Mkuu wa TEC Padri Raymond Saba.
“Semina hii
iwasaidie na ninyi mkaandae semina kama hizi huko majimboni. Tukumbuke kuwa
mambo haya ya fedha na miradi yanagusa taasisi ambazo majimboni kwetu ziko
nyingi. Kwa hiyo sisi tunalo jukumu la kufikisha ujuzi huu katika ngazi ya
chini kabisa, ikiwezekana hata katika jumuiya ndogo ndogo” Padri Chrisantus
Ndaga, Naibu Katibu Mkuu AMECEA. (Na Pascal Mwanache)
Comments
Post a Comment