Mbaroni kwa kuteketeza mabweni ya seminari ya St.Mary’s,Mbeya
n Na Thompson Mpanji, Mbeya
Baada
ya uchunguzi wa Seminary Ndogo ya St. Mary’s Mbeya pamoja na polisi kuhusu
chanzo cha moto ulioteketeza mabweni mawili ya Seminari hiyo kwa nyakati
tofauti mtuhumiwa wa tukio hilo amekamatwa na kutiwa mbaroni.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinasema kuwa baada ya
matukio yote mawili Uongozi wa shule ya St.Mary’s Mbalizi uliamua kuimarisha
ulinzi shirikishi kwa wanafunzi wenyewe kuwekeana zamu na hivyo
kufanikiwa kuwanasa vijana wanne wanaodaiwa kukutwa na dumu la mafuta
yanayodhaniwa kuwa ni petroli majira ya usiku wakitaka kuchoma moto
majengo mengine wakati wanafunzi wakiwa wamelala.
Aidha taarifa hizo zinasema kuwa vijana watatu walifanikiwa
kutoroka kusikojulikana na kubakia na kijana mmoja ambaye ametiwa
mbaroni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Naibu Kamishna Mpinga amethibitisha
kukamatwa kwa kijana huyo (jina limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) mwenye
umri wa miaka 12 ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha awali katika
seminari hiyo siku ya jumamosi Februari,3,2018 na baada ya mahojiano amekiri
kuhusika kutenda matukio yote mawili ya kuteketea kwa mabweni hayo.
“Tumefanikiwa kumkamata kijana mmoja siku ya
jumamosi alikuwa mwanafunzi wa pre form one katika shule hiyo ambaye kwa
sababu za kiuchunguzi na kiusalama jina linahifadhiwa na
amekiri kuhusika katika matukio yote mawili kutokana na shinikizo la mtu mmoja
aliyemtishia kuwa asipotekeleza uhalifu huo atamkata na mapanga,kwa hiyo
tunamshikilia na tunaendelea na uchunguzi zaidi”amehitimisha Kamanda Mpinga.
Comments
Post a Comment