Posts

Showing posts from August, 2018

‘Ukristo ni vita’ Ask. Amani

Image
Na Erick Paschal, Moshi WAKRISTO wakatoliki nchini wametakiwa kutambua kuwa ukristo ni vita na mapambano ambapo maisha ya hapa duniani ni ya muda kwa ajili ya kujiandaa na maisha ya milele. Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu Isaac Amani wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha wakati akitoa homilia yake kwenye adhimisho la Misa Takatifu ya kilele cha Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara kanda ya kaskazini, Misa iliyoambatana na sherehe ya Bikira Maria mpalizwa mbinguni. Askofu Amani amesema kuwa mpango wa Mungu mara zote ni kumuokoa mwanadamu, na maovu anayoyatenda mwanadamu yanakwenda kinyume na mpango wa Mungu, kwa kuwa Mungu anashughulikia wokovu kwa sababu binadamu ana thamani mbele yake. Askofu Amani amesisitiza kuwa kila mwanadamu hana budi kujitathmini na kujichunguza kwani mpango wa Mungu siku zote ni wokovu hivyo kila mmoja ana wajibu wa kujiuliza kama ni wakala wa Mungu ama wa shetani kwa matendo. Vijana ni zamu yenu kuwa wamisionari Wakati huo huo vijana n

‘Jubilei ni azimio la kuanza upya wa maisha, siyo idadi ya miaka’

Image
Na Pascal Mwanache, Imiliwaha I MEELEZWA kuwa jubilei siyo tu idadi ya miaka fulani, bali ni azimio la kuanza upya wa maisha katika kuelekea ukamilifu na utakatifu. Hayo yamesemwa na Abate wa Abasia ya Hanga-Songea, Abate Octavian Masingo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 50 ya Shirika la Masista wa Mtakatifu Agnes-Chipole, Nyumba ya Mtakatifu Getrude Imiliwaha. Akitoa homilia katika adhimisho hilo Abate Octavian amesema kuwa katika kipindi cha jubilei masista hao hawana budi kuweka mikazo na mikakati thabiti kuelekea katika kilele huku mkazo ukiwekwa katika kutathmini hali halisi ya wito wao badala ya kujikita katika kuhangaikia vitu. “Mnapoizindua jubilei hii mnaazimia kuanza upya maisha yenu ya kiroho. Inawapasa kunuia kuelekea katika utakatifu na ukamilifu” ameeleza. Aidha ameongeza kuwa maandalizi ya kuelekea kilele cha jubilei hiyo hayapaswi kujikita katika vitu kwani kufanya hivyo ni kupotosha dhamira ya kumshukuru M

‘Mwanakwaya mwenye vikwazo vinavyomtenga na ekaristi hataruhusiwa kuimba’

Image
Na Marco Kanani, Geita WITO umetolewa kwa wanakwaya wote wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Fatima Geita kuhakikisha wanakuwa mfano hai wa kupokea masakramenti, ambapo hadi kufika juma la kwanza la majilio kila mwanakwaya ambaye atakuwa hajarekebisha ndoa au kuondoa kikwazo chochote kinachomtenga na sakramenti za Kanisa hataruhusiwa kuimba. Wito huo umetolewa na Padri Gerald Singu Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Fatima Geita wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu akiwa anaongea na waamini wa Parokia hiyo katika mahubiri yaliyoenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Vijana Kijimbo. Padri Singu mesema kuwa haiwezekani mwanakwaya ahamasishe waamini katika nyimbo kwenda kukomunika wakati yeye anabaki amekaa kwenye kiti.   Pia ametoa rai kwa viongozi wa ngazi mbalimbali za kanisa katika parokia hiyo kuanzia ngazi ya jumuiya kuwafikia waamini wote wasiopokea masakramenti kuwafikia na kuwashauri kurudia masakramenti, wawape miongozo itakayowafanya waone ni jambo jema kwa