Ask. Chengula: Wazazi wa mapadri mfahamu upadri si mali
ASKOFU wa Jimbo
Katoliki Mbeya ametoa wito kwa jamii na wazazi wanakotokea
mapadri kuwaombea wapate nguvu za utume badala ya kuwatwika mizigo ya kudai
mali.
Askofu
Chengula amesema hayo wakati akitoa Daraja Takatifu la Upadri kwa Shemasi Cleophas Sukari katika Kanisa la Hija Parokia
ya Mwanjelwa.
Amewasihi
wazazi wanaowatoa watoto wao katika
kulitumikia Kanisa kama mapadri kuendelea kuwaombea watoto wao waweze kuishi
vyema upadri wao na wamtumikie Mungu ipasavyo.
“Wazazi
mvumilie maana watoto wenu wanamtolea Mungu sadaka na kutakatifuza watu. Hawana
mali za kuwapa kwani upadri hakuna mali,ni kujitoa kwa Kanisa.
Hakuna
mshahara wala posho,wala hakuna madini,kwa hivyo wazazi mnapowatoa watoto
wenu mufahamu kuwa mnayo kazi kubwa ya
kuendelea kuwasaidia na kuwalea kwa
ujumla wao,”amesema.
Aidha
Askofu Chengula ametaka mapadri kufuatilia kwa ukaribu waamini katika jumuiya zao kujua changamoto zao za kiimani, wenye shida
mbalimbali na kuwasaidia inapowezekana
ili wakue kiimani wasisubiri waamini wawafuate maparokiani.
Comments
Post a Comment