Askofu Kinyaia aonya waamini wanaoamini ushirikina
ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu
Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaia,
amewataka wakristo kuacha tabia ya kukimbilia kwa waganga wa kienyeji
wanapopatwa na matatizo mbalimbali ya maisha.
Ameyasema hayo katika Ibada ya Misa Takatifu alipokuwa anatoa Sakramenti ya Kipaimara kwa
vijana 190 katika Parokia ya Mt.Maria
Imakulata-Bihawana Jimbo Kuu Katoliki
Dodoma.
Askofu Kinyaia amesema kuwa wakristo wanapaswa kujenga
mazoea ya kupeleka matatizo na shida zao kwa Mungu na sio kwa Sangoma yaani
waganga wa kienyeji kwani ni kinyume na imani yao.
“Vijana wanaopata Sakramenti ya Kipaimara wanapaswa
kuendelea na malezi ya karibu kutoka kwa wazazi na jamii.
Kanisa pia lina jukumu la kutoa malezi endelevu ili
kuwasaidia kusimama imara katika imani. Tukizembea hawa ndio watakaokuwa
waganga wa kienyeji ama kuamini imani za kishirikina,” amesema Askofu Kinyaia.
Amewaasa vijana hao pamoja na waamini wote kupokea
Sakramenti mbalimbali za Kanisa kujitakatifuza na kutumia vipaji vyao kutumikia
jamii.
Waamini hao 190 waliopata Sakramenti ya Kipaimara
wanatoka katika vigango vigango 13 vya Parokia ya Bihawana.
Comments
Post a Comment