Posts

Showing posts from May, 2018

PAPA AMEMTEUA PADRI ANTHONY LAGWEN KUWA ASKOFU WA MBULU

Image
Mh. Pd. Anthony Lagwen ateuliwa kuwa Askofu Jimbo Katoliki la Mbulu Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Anthony Lagwen kutoka Jimbo Katoliki la Mbulu, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Mbulu, nchini Tanzania. Askofu mteule Anthony Lagwen alizaliwa tarehe 5 Julai 1967 huko Tlawi, Jimboni Mbulu. Baada ya masomo yake ya msingi, alibahatika kuendelea na masomo ya sekondari katika Seminari Ndogo ya Sanu, Jimbo Katoliki la Mbulu. Akapata masomo ya falsafa kutoka Seminari kuu ya Ntungamo, iliyoko Jimbo Katoliki la Bukoba na baadaye akahamia Seminari kuu ya Kipalapala, Jimbo kuu la Tabora ili kuendelea na masomo ya kitaalimungu. Tarehe 18 Oktoba 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki Mbulu. Tangu wakati huo, katika maisha na utume wake wa Kipadre kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2000, alikuwa Paroko-usu wa Parokia ya Bashay. Kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2004 akepelekwa na Jimbo kujiendeleza zaidi katika masuala ya biashara kwenye Chuo Kikuu cha Mtaka

Suluhu ya maadili kwa mapadri, wanandoa ni malezi kwa vijana

Image
Na Sarah Pelaji, Dar es Salaam A skofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Flavian Kassala ameiasa jamii kuwekeza kwenye malezi kwa vijana ili kutatua changamoto zilizopo katika ndoa, upadri, utawa na katika nyanja zote za jamii. Akizungumza na Gazeti Kiongozi, Askofu Kassala amesema kuwa, ulimwengu wa sasa umegubikwa na changamoto mbalimbali kwasababu jamii inazembea malezi kwa watoto na vijana. “Miito mitakatifu ya Ndoa, Upadri, utawa inaitikiwa na watu ambao wapo tayari kuelekezwa, kutengenezwa na kulelewa ili wamudu maisha waliyoitiwa na Mungu. Upadri pamoja na kuwa ni wito bado unahitaji malezi, uelekezi na kumtengeneza kijana aweze kuwa padri anayehitajika katika jamii. Analelewa ili awe na tabia zenye utu ndani mwake , upendo, wema, uwajibikaji, uchaji wa Mungu nk. Seminari hazipokei watu wakamilifu, watu ambao tayari wameshatengenezwa (ready made) hapana ndiyo maana kuna muda wa malezi    ili kijana apate malezi ya kuweza kuuishi upadri wake. Changam

Waamini msiwamiliki mapadri - Askofu Kassala

Image
Na Marco Kanani, Geita W AAMINI wameonywa kutowamiliki Mapadri na Mashemasi na kuwafanya kushindwa kutimiza vyema majukumu yao. Wajibu wao ni kuwaombea kwa Mungu ili utume wao uweze kuwa mwema mbele za Mwenyezi Mungu na kulistawisha Kanisa katika utumishi uliotukuka. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Askofu   Flavian Kassala wa Jimbo Katoliki la Geita wakati akitoa Daraja Takatifu la Ushemasi kwa Frateri Didas Kahigi katika Parokia Teule ya Nyehunge jimboni Geita. Askofu Kassala amesema kuwa, si sawa waamini kuwamiliki Mapadri na Mashemasi kwani ni sawa na kuliangamiza Kanisa kwani kutawafanya watumishi hao wa Mungu kushindwa kutimiza vyema majukumu yao pale watakapokubali kuwa miliki ya baadhi ya waaamini. Aidha amesisitiza kuwa jambo hilo si jema pia machoni pa Mungu . Amewahiza waaamini wote kuacha kabisa tabia ya kutamani kuwamiliki Mapadri na Mashemasi huku wakijua wanalo jukumu kubwa la kuwafikia waaamini wote bila kuwabagua ili kuwaelekeza njia