‘Wakatoliki ishini ukatoliki wenu’
WAAMINI wa Kanisa
Katoliki wametakiwa kuishi maisha yaliyo mema katika Familia, Jumuiya , mitaa
yao pamoja na jirani zao, ili Mwenyezi Mungu aweze kuidhihirika ndani mwao kila
siku za maisha yao.
|
Hayo
yameelezwa na Makamu wa Askofu wa jimbo
Katoliki la Iringa ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Ifunda Padri, Vicent Mwagala wakati wa mahubiri yake kwa Waamini
wa Parokia hiyo wakati akiadhimisha Sadaka ya Misa Takatifu ya kupaa Bwana.
Padri
Mgwagala amesema kuwa, Mungu kamwe hawezi kujitenga nao na daima yuko kati yao
kupitia Roho Mtakatifu ,ambaye anawaangazia ili Kristo aliyepaa Mbinguni
aendelee kuishi ndani yao, kwani katika Kristo Waamini Wote wanatumaini
kuufikia ufamle wa mbingu.
Ameongeza
Kuwa zawadi ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Mungu inawasaidia Waamini kutambua
kuwa, wao wameunganika na Kristo aliyekichwa cha Kanisa, na kupitia kwake ndipo
nao wataweza kufika mbinguni kwa Baba, lakini ili waweze kufika huko ni lazima
wajibidishe.
Aidha
Padri Mwagala ameeleza kuwa, Waamini wanapaswa kutambua kuwa wao ni tabernakulo
pale wanapompokea Yesu Kristo wakiwa katika hali iliyo njema, kwani Yesu Kristo
anaingia ndani mwao mzima na Mungu kweli, na hivyo wanatakiwa kuwaka daima moto
wa mapendo, kama vile taa ya milele inavyowaka mbele ya Yesu wa Ekaristi.
Padri
Mwagala amehitimiha mahubiri yake kwa kuwata, kuendelea kumuomba Mama Bikira
Maria ili awe msaada kwao, na pia aendelee kuwaombea kwa mwanae, ili waweze
daima kutambua uwepo wake katika neno
lake, huku nawao wakikubali kujitoa sadaka katika kuwasaidia wale wote
wanaohitaji msaada wao.
Comments
Post a Comment