Maaskofu wa Chile wakutana na Papa mkutano wa dharura
MAASKOFU
wa Chile wapo Roma wiki hii kwa ajili ya mkutano wa dharura na Papa Fransisko,
ambaye anataka kukabiliana na mgogoro wa unyanyasaji wa kijinsia uliojificha
katika Kanisa nchini mwao.
|
Maaskofu thelathini na moja wa Chile watashiriki,
pamoja na wachache waliostaafu.
Mkutano huo
utaanza Mei 15-17 ambapo Kardinali Cardinal Francisco Javier Errázuriz wa Chile
anahusika zaidi na mzozo huo kwani
anashutumiwa na waathirika wa unyanyasaji na Mahakama ya Jinai ya Vatikani
kufunika kesi ya Padri Fernando Karadima, ambaye alikuwa kuhani maarufu nchini
Chile, baada ya kupata hatia ya unyanyasaji wa kijinsia miaka kadhaa iliyopita.
Taarifa
kutoka Vatikani zimeeleza kuwa, mkutano utafanyika kwa siri, na kwamba Baba
Mtakatifu angewasilisha maaskofu wa Chile kwa hitimisho lake kwa misingi ya
hati ya 2300 ya uchunguzi wake maalum.
Maaskofu wa
Chile wanasema kuwa, makosa yalifanyika wakati wa kushughulikia kesi za
unyanyasaji wa kijinsia wakati huo.
Askofu Fernando Ramos wa Chile amesema
maaskofu wa Chile wameona ‘maumivu na aibu’ kuhusu unyanyasaji wa kijinsia
uliofanywa na viongozi wa Kanisa nchini Chile.
“Sisemi
kwamba labda tumefanya makosa, la hasha! Tumefanya makosa, “amesema Askofu Juan
Ignacio Gonzalez Errazuriz wa Jimbo la San Bernardo Chile.
Askofu
Gonzalez, pamoja na Askofu Msaidizi Fernando Ramos Perez wa Santiago, wamesema
hayo wakati walipokutana na waandishi wa habari Mei 14 mwaka huu Roma
walipohudhuria mkutano huo wa siku tatu .
Akijibu
barua ya Papa Aprili 11 mwaka huu kwa Maaskofu wa Chile, Askofu Ramos
aliwaambia waandishi wa habari kuwa maaskofu waliona “maumivu na aibu” kwa
sababu ya uhalifu uliofanywa na viongozi wa Kanisa.
“Kupokea
habari kwamba unyanyasaji wa kijinsia ulifanyika katika jumuiya yetu
iliwashangaza watu wengi kwasababu ni kitu ambacho hakikubaliki na hakivumiliki.
Walipoulizwa
kama wana nia ya kufuata maongozi wa Papa na kuomba msamaha kwa waathirika,
maaskofu hao walisema hawawezi kuacha kuomba msamaha kutokana na majeraha
waliyofanyiwa waathirika hao ni ni
sharti la maadili,” amesema Askofu Ramos .
“Kama Yesu
alisema, tunapaswa kuomba na kutoa msamaha saba mara 70, tuna hakika kwamba
tutaomba msamaha na tunatarajia kusamehewa.
Hivi
karibuni, waathirika watatu wa unyanyasaji wa kijinsia kutoka Chile walikutana
na Papa Fransisko kumueleza juu ya unyanyasaji wa kijinsia waliofanya viongozi
wa Kanisa nchini Chile mika kumi iliyopita.
Awali Papa
Fransisko alimualika Juan Carlos Cruz,
Jose Andres Murillo na James Hamilton kukaa katika Domus Sanctae Marthae,
makazi ya Vatikani ambako anaishi, ili wakutane naye peke yake kuanzia Aprili
27 mpaka 29 mwaka huu. Walikutana naye tena kama kikundi Aprili 30 .
“Kwa miaka
10 tumehukumiwa kuwa maadui, kwa sababu tunapinga unyanyasaji wa kijinsia
uliojificha ndani ya Kanisa.”
Cruz amesema
alimueleza Papa jinsi alivyotukanwa na Kardinali Francisco Javier Errazuriz
Ossa, Askofu Mkuu Mstaafu wa Santiago na
mrithi wake Kardinali Riccardo Ezzati, katika barua pepe.
“Nilishuhudia
watu hawa wawili jinsi wahakuwa na heshima kwa mtu na kumnyanyasa na
unyanyasaji huo ulikuwa unayojulikana kwa sababu ndivyo walivyomfanyia Jimmy
(Hamilton) na Jose (Murillo) na vyombo vya habari viliripoti.
Waliniita
‘nyoka,’ waliniita kila kitu, kwasababu tu ya kusema ukweli,” Cruz alimueleza
Papa.
Alipoulizwa
ikiwa walipata msamaha kutoka kwa maaskofu wa Chile, Cruz alisema: “Papa
Fransisko aliomba msamaha mwenyewe na kwa niaba ya Kanisa zima. Maaskofu wa
Chile hajui kuomba msamaha.“
Askofu
Gonzalez aliwaambia waandishi wa habari kuwa waathirika hao lazima wabaki
katikati ya majadiliano yenye ukweli.
Muda mfupi
baada ya mkutano na waandishi wa habari, Cruz aliandika hivi: “Sijawahi kumwona
Papa kabla ya maisha yangu. Ukweli kulingana na maaskofu wa Chile ni tofauti
sana na yale tunayoishi. “
“Hitimisho
langu kuhusu mkutano wa waandishi wa maaskofu wa Chile - (Maaskofu) Ramos na
Gonzalez - ni kwamba wanajua ukweli na wanapaswa kurudi kwenye sayari kujirudi
na kuomba msamaha, “ Cruz alisema katika tweet .
Comments
Post a Comment