Posts

Showing posts from January, 2020

Tanzania yachukua hatua kukabiliana na nzige

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Tanzania inashiriki kusaidia kupoteza nzige walioibuka na kushambulia mashamba nchini Kenya ili wasiongezeke tatizo likawa kubwa zaidi lakini pia lisije likahamia nchini Tanzania. Majaliwa alisema hayo bungeni jijini Dodoma eo Alhamisi Januari 30, alipokuwa kijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi aliyetaka kujua namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na wadudu hao. “Hili baa la nzige ambalo tayari limeshafika katika baadhi ya nchi jirani hasa za Afrika Mashariki, nilikuwa napenda kufahamu, serikali imejipangaje katika kukabiliana na kudhibiti masuala haya?” amehoji. Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema kuhusu nzige ambao jirani zetu mazao yao yanaharibiwa, ni wadudu hatari ambao wakiingia nchini watamaliza mazao yetu hivyo serikali imemechukua tahadhari ambapo Wizara ya Kilimo inaendelea kuwasiliana na Wizara ya Kilimo nchini Kenya kuona mwenendo na ukuaji wa tatizo hilo. “Na sisi huku tunajipanga kwa namna ambavyo tunaw

Askofu Amani awapongeza watawa wa Shirika jipya Arusha walioweka nadhiri

Image
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki   Arusha Mha. Isaac Amani, ameitaka jamii kuwa tayari na kufanya maandalizi ya kina katika kuitikia na kuuchuchumilia wito wowote wa maisha wa kuwatumikia watu kadri ya mpango wake   Mungu Mwenyezi. Rai hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki jimboni humo akiihubiria hadhira ya waamini waliofurika katika Kanisa la Mt. Yokobo Mtume Parokiani Moshono kwenye sherehe za kuweka nadhiri za kwanza za kitawa kwa masista watatu wa kwanza wa Shirika jipya la Kimisionari la Ekaristi Takatifu na Uinjilishaji Mpya. Askofu Mkuu Amani amefafanua kuwa wito uwe wa maisha mathalani;   ndoa, utawa na upadri au wa kitaaluma na wa kiuongozi chimbuko lake ni Mwenyezi Mungu mweyewe anaeanzisha na kumwita mtu kutumika ipasavyo na wala si kutumikiwa. “Mwenye kuita ni Mungu na mwenye kuitwa ana kazi tatu kuu, mosi kuisikia sauti ya Mungu, pili kuitikia kwa kuikubali na kuishi agizo la Mungu na tatu ni   kufikisha ujumbe wa Mungu kwa watu kwa ajili ya maendeleo yao ya kiroho,

Uhai wa Kanisa si wingi wa mapadri, waamini, watawa

Image
Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi Mhashamu Askofu Filbert Felician Mhasi amewakumbusha waamini kuwa uhai wa Kanisa siyo wingi wa waamini makanisani, waseminaristi maseminarini, watawa katika nyumba za kitawa bali ni maisha yao ya Imani wanayoyaishi. Rai hiyo   ameitoa hivi karibuni akiongoza Misa Takatifu   katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo Mtume Kipalapala Tabora akitoa huduma ya usomaji Masomo kanisani na huduma altareni kwa mafrateri wa mwaka wa pili na watatu. Askofu huyo amesema uhai wa Kanisa hautegemei wingi wa mafrateri katika seminari na swali muhimu ni   Je, wanastahili? Aidha Askofu Mhasi amesema Upadri unajengwa katika maisha imara ya Ukristo, tunakuwa wakristo kabla ya kuwa mapadri hivyo ni wajibu   wa kila mkristo kuishi imani yake kwa uaminifu. Amewakumbusha mafrateri hao kuwa mabalozi kule waendako baada ya kuwa mapadri. Maisha ya Upadri ni sawa na mbio za kijiti, watu tunapasiana kila mmoja kwa wakati wake na stamina yake, ni vema zamu yako ikifik