Posts

Showing posts from 2016

Maaskofu watoa angalizo kuhusu mwelekeo wa nchi

Image
·       Wahimiza utawala wa sheria, haki, amani na uwajibikaji ·       Watahadharisha kukithiri kwa uharibifu wa mazingira KATIKA kusherehekea Sikukuu ya Noeli nchini, baadhi ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania wamewataka watanzania kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani, upendo, umoja na mshikamano wa kitaifa, na kuachana na matendo ya giza yanayosababisha rushwa, ufisadi na utendaji wa kazi unaofanywa kwa mazoea. Akitoa homilia yake katika Misa ya Krismasi ndani ya Kanisa la Bikira Maria wa Fatima lililopo Geita, Askofu Flavian Kassala wa Jimbo Katoliki Geita amesema kuwa kila mtanzania anapaswa ajione kuwa ni chanzo cha amani. Askofu Kassala ameonya kuwa   kisiwepo kisingizio chochote kwa mtu yeyote kuvuruga amani ya nchi ambayo imekuwa zawadi kubwa na ya kipekee kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ametoa mfano wa nchi zilizo katika vita, ambako watu wanavyoishi kwa shida kubwa huku maelfu ya watu wakipoteza maisha, na hivyo akatoa wito kila mtu kuhak

WARAKA MZITO WA BABA ASKOFU SEVERINE NIWEMUGIZI KWA WATANZANIA HUU HAPA..

Image
Heri ya Krismasi! Tunaadhimisha sherehe za kuzaliwa Bwana Yesu Kristo mwaka huu 2016 kukiwa na hisia na mitazamo mbali mbali ya watu wa makundi tofauti katika jamii yetu, juu ya hali ya maisha ya mtanzania leo. Hii ni hasa baada ya kusikia toka kwa watu mbali mbali tathmini za hali halisi ilivyo mijini na vijijini. Licha ya tetemeko la ardhi lililotikisa huku Kagera mwezi Septemba na njaa pia katika baadhi ya wilaya mkoani Kagera, baadhi ya watumishi wa umma hasa waliozoea kufanya kazi kwa mazoea na bila kuzingatia nidhamu na maadili ya utumishi wao wameishi kwa hati hati wasijue kutumbuliwa kwao kutakuwa lini na tokea wapi! Wafanya biashara nao biashara zao zimepiga miayo kwa sababu ya kutochanganya kama ilivyozoeleka huko nyuma, wengi wanasema hali ni ngumu, pesa haikamatiki! Viongozi wa makanisa nasi tumejikuta tukikimbizana na viongozi wa serikali kuulizana nao kama ubia wa sera ya PPP (Public-Private-Partnership) bado unaishi au la. Milango yao na masikio havikufunguli

Askofu Rwoma: Msitoe wala kushiriki kutoa mimba

Image
Askofu wa jimbo katoliki Bukoba Mhashamu Desiderius Rwoma amewataka wanawake wote wakristo nchini kukataa kupokea shinikizo lolote la kutoa mimba wakiiga mfano wa Bikira Maria alivyokubali kumleta duniani Mkombozi wao Yesu Kristo. Askofu Rwoma ametoa rai hiyo wakati wa mahubiri yake kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kwenye   adhimisho la misa takatifu ya Krismasi kitaifa iliyofanyika katika kanisa kuu la jimbo katoliki Bukoba. “Kataeni aina yoyote ya ushawishi ama sababu zozote zile ambazo zinaweza kuwasukuma kukubali kutoa mimba, ukitoa mimba licha ya kumkosea Mwenyezi Mungu na kiumbe kisicho na hatia, pia umelikosesha taifa pengine mtu ambaye angechangia katika maendeleo yake,” amefafanua. Amesema Yesu Kristo aliyezaliwa ni mkombozi wa kila mtu, hivyo kuzaliwa kwake ni furaha kubwa na wakristo hawana budi kusherehea kwa kufurahi kwani imefunuliwa neema ya Mungu inayowakomboa wote. “Krismasi ni kipindi cha neema na fursa adhimu ya kufurahi, kubak