Fumbo la Umwilisho linamwezesha Mungu kuwa kati na watu wake!

Mwenyezi Mungu kwa njia ya Fumbo la Umwilisho amekuwa karibu sana katika maisha ya mwanadamu, tema ambayo ni kiini cha Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya nne ya kipindi cha Mwaka A wa Kanisa. Wahusika wakuu katika Fumbo hili ni Bikira Maria na Mchumba wake Yosefu. Hili ni fumbo la upendo na uwepo wa Mungu kati ya wanadamu! Haya yamesemwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili tarehe 18 Desemba 2016.
Bikira Maria katika mwanga wa Unabii ndiye atakayechukua mimba na kumzaa Mwana wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Neno wa Mungu anafanyika mwili na kuwa kama binadamu na kupokelewa na Bikira Maria, kama ilivyo pia hata kwa waamini wengine, Mwenyezi Mungu anapowaendea na kuwakirimia neema na baraka katika maisha yao! Hapa jambo la msingi ni kujiuliza ikiwa kama waamini wanamfungulia Mungu malango ya maisha yao, au wanaamua kumfungia nje kutokana na matendo yao.
Bikira Maria alijitosa bila ya kujibakiza ili kushiriki kikamilifu katika historia ya Ukombozi kwa kusaidia mchakato wa kuleta mabadiliko katika maisha ya mwanadamu. Hivi ndivyo inavyokuwa hata kwa waamini wengine wanapokubali kumpokea na kufuata nyayo za Kristo Yesu, wanaweza kushiriki katika ukombozi wao binafsi na kwa ajili ya jirani zao. Bikira Maria ni mfano bora wa kuigwa katika kumwangalia na kumtafuta Mwenyezi Mungu, katika uwepo wake wa karibu katika maisha ya binadamu, kwa kumwachia nafasi ili aweze kuingia katika majukumu yao na hatimaye kuwasaidia kujenga utamaduni wa upendo.
Mwinjili Mathayo anamwonesha Mtakatifu Yosefu mtu wa hakikwani ni kati ya wahusika wakuu katika Fumbo la Umwilisho kwani katika maisha yake anapata hofu na mashaka na kushindwa kuyapatia majibu muafaka mahangaiko yake ya ndani, yaani kwa kumwona Bikira Maria akiwa ni mjamzito. Katika kipindi hiki cha giza na mahangaiko ya ndani, Mwenyezi Mungu kwa njia ya mjumbe wake anamwendea Mtakatifu Yosefu na kumpatia mwanga wa Fumbo la Umwilisho kwamba, Mtoto atakayezaliwa ni kwa njia ya Roho Mtakatifu; ujumbe ambao bado uliendelea kumwachia maswali yasiyokuwa na majibu, lakini hatimaye akajiachilia mikononi mwa Mwenyezi Mungu na kumpokea Bikira Maria kuwa mke wake.
Mtakatifu Yosefu kwa kumkubali na kumpokea Bikira Maria anamkubali na kumpokea Neno wa Mungu aliyetungwa mimba kwa njia ya Roho Mtakatifu, kwani mbele ya Mwenyezi Mungu hakuna lisilowezekana. Mtakatifu Yosef uni mtu wa haki na mnyenyekevu asiye kuwa na makuu anayewafundisha waamini kujiaminisha mbele ya Mwenyezi Mungu, ili aweze kuwaongoza na hivyo kutekeleza mapenzi yake kwa utii pasi na shuruti.
Baba Mtakatifu Francisko anakaza kusema, Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu walikuwa ni watu wa kwanza kumpokea Kristo Yesu kwa njia ya imani na hivyo wanawaingiza waamini wengine katika Fumbo la Umwilisho, yaani kuzaliwa kwa Mkombozi, wakati wa Siku kuu ya Noeli. Bikira Maria ni mfano bora wa kuigwa kwa majitoleo ili kumpokea na kumkaribisha Mwana wa Mungu katika uhalisia wa maisha. Mtakatifu Yosefu anawasaidia waamini daima kutafuta mapenzi ya Mungu katika maisha yao na kuyatekeleza kwa imani kamili. Wote wawili walijiachia mikononi mwa Mungu na Mwenyezi Mungu akawakaribia.
Bikira Maria atachukua mimba na kumzaa Mtoto atakayeitwa Immanueli maana yake Mungu pamoja nasi, yaani Mungu yu karibu sana na watu wake, mwaliko kwa waamini kumfungulia Mungu malango ya maisha yao, kwa kumsikiliza kutoka katika undani wao; katika huduma kwa jirani na wakati wa sala. Haya ni matukio ambayo kwayo Mungu anakuwa karibu sana na waja wake. Huu ndio ujumbe wa matumaini unaotekelezwa wakati wa Siku kuu ya Noeli. Mwishoni, Baba Mtakatifu Francisko anasema matumaini ya ujio wa Mungu yanapata utimilifu wake kati ya watu, Kanisa na kati ya watu wadogo ambayo ulimwengu unawanyanyasa, lakini mbele ya Mwenyezi Mungu wanapendwa sana na Mungu daima anakuwa karibu nao!
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

Comments

  1. Ninamshukuru sana Dk dawn acuna, aliandika uchawi wa mapenzi ambao ulimrudisha mpenzi wangu wa zamani katika masaa 48, shukrani kwake, ikiwa una hali kama hiyo.
    *Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
    *Kama unataka kupata mimba.
    *Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
    Ikiwa unataka kuponya aina yoyote ya ugonjwa. Na wengine,
    Wasiliana naye yeye ndiye mtu sahihi wa kutatua tatizo hili.
    Barua pepe: { dawnacuna314@gmail.com }
    Whatsapp: +2348032246310

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU