Salam za matashi mema kwa Papa Francisko kutoka Afrika!

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM kwa niaba ya familia ya Mungu Barani Afrika, linapenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya Baba Mtakatifu Fransisko anapoadhimisha kumbu kumbu ya miaka 80 tangu kuzaliwa kwake. Familia ya Mungu Barani Afrika, inamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kusimama kidete: kulinda, kutetea na kudumisha Injili ya familia na kwamba, SECAM kwa upande wake, itaendelea kujizatiti kwa ajili ya kutangaza, kudumisha na kushuhudia tunu msingi za maisha ya ndoa na familia.


Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar  kwa mara nyingine linamtakia heri, baraka na maisha marefu Baba Mtakatifu Francisko katika utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Aendelee kutekeleza dhamana na majukumu yake kwa uaminifu, uadilifu, imani, mapendo na matumaini. Ujumbe wa SECAM umeandikwa Askofu Emmanuel Adetoyese Badejo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, CEPACS.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU