WAHITIMU ZAIDI YA 2000 CHUO KIKUU SAUT JIJINI MWANZA KUTUNUKIWA VYETI MBALIMBALI WIKENDI HII


Wahitimu 2421 wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada, shahada za uzamili na uzamivu katika mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine SAUT cha Jijini Mwanza.

Makamu Mkuu wa chuo hicho Dkt.Thadeus Mkamwa amesema wahitimu hao wakiwemo watatu wa shahada za uzamivu watatunukiwa shahada zao kwenye Mahafali yatakayofanyika ijumaa na jumamosi wiki hii chuoni hapo.

Amesema mahafali hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza Mhashamu Yudatadei Rwaichi yatatanguliwa na Siku ya Maonesho Kitaaluma yatakayohusisha wanafunzi na wahadhiri kutoka kila kitivo na idara.

Hata hivyo Dkt.Mkamwa amesema wanafunzi 746 wameshindwa kuhitimu masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kulipa ada.




Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU