Serikali Mara kushirikiana na Kanisa Katoliki kuikabili njaa

SERIKALI Mkoani Mara imesema alisema kuwa suluhisho la tembo kuharibu mazao yakiwa ghalani limepatika kwani Serikali itashirikiana na chuo  cha ufundi  cha Mt. Antony kuwahamasisha wananchi waweze kununua vihenge hivyo ambavyo tembo hawezi kuharibu mazao yakiwa ghalani .

Hiyo ni moja ya mbinu ya kunusuru hali ya njaa inayowakabili wananchi wa Mkoa huo kutokana na tembo kula mazao yakiwa shambani na hata baada ya kuvunwa yakiwa ghalani.

Akizungumza kwenye mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi cha Mt. Antony kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma , yaliyofanyika Chuoni hapo,Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi alisema kuwa  amefurahishwa sana  kuona vihenge vya chuma   vinavyotengenzwa Chuoni hapo vyenye uwezo wa kubeba tani 2 kwa wakati mmoja.


“Mimi siamini kabisa kama tembo anaakili kumzidi binadamu na ninashangaa sana kila mtu analalamikia tembo tembo imekuwa kama wimbo,lakini baada ya kutembelea maeneo ya chuo hiki na kujionea shughuli za ufundi mbalimbali zinazofanywa na chuo hiki nimefurahi sana na moja kwa moja nikaona suluhisho la kilio cha wananchi kuhusu tembo nimekipata na sasa kilichobakia ni uhamasishaji tu watu watumie vihenge hivi vya kisasa kuhufadhi chakula kuanzia ngazi ya kaya,” alisema Dk Mlingwa.

Aidha ameahidi kushirkiana na chuo hicho katika kutatua changamoto zinazokikabili chuo hicho na kusema kuwa chuo hicho ni kikubwa sana katika mkoa huo na kinauwezo wa kuchukua wanafunzi wengi kwa kozi mbalimbali,wakati wanaendelea na mchakato wa kujenga vyuo vingine.
Amelihakikishia Kanisa kuwa, serikali  itashirikana na Chuo cha Ufundi cha  Mt. Antony katika  kufundisha mbinu za kilimo cha nafaka, na kuboresha uhifadhi wa chakula kuanzia ngazi ya kaya ,kwa kutumia vihenge vya kisasa vinayopatikana katika Chuo hicho ili kukabiliana na tembo ambao wamekuwa wakiharibu chakula kikiwa ghalani.

Mkuu wa Chuo hicho Sista Rozina Kimaro alisema kuwa  jumla ya wahitimi 43 wamehitimu katika kozi mbalimbali,na hadi sasa chuo hicho kimeshatoa wanafunzi 2392  wamehitimu mafunzi ya hao wahitimu wapatao 610 wameajiliwa na wahitimu 940 wamejiajili wenyewe tangu kianzishwe mwaka 1997 na hivyo kupunguza  idadi ya vijana wasio na ajira katika jamii.


Sista Kimaro alisema kuwa changamoto kubwa ambayo chuo inakabilana nacho kwa sasa ni wafadhili kutoendelea kutoa msaada ,hivyo vijana ambao ni yatima  na wale wa mazingira magumu M,Kwaliokuwa wakisaidiwa kutoendelea kusaidiwa tena kutokana na uwezo wa chuo kutoweza na ndoto zao kudidimia.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU