Ask. Minde awataka waamini kijiandaa kumpokea Mtoto Yesu.




ASKOFU Ludovick Minde wa Jimbo la Katoliki Kahama amewataka waamini   kujitakasa na kujiandaa kiroho  katika kipindi hiki cha maajilio  ili waweze  kumpokea kwa moyo safi  Masiha   Yesu Kristo.

Askofu Minde  ametoa wito huo hivi karibuni katika Misa  Takatifu  alipokuwa akizinduzia  Parokia  Teule  ya Utatu Mtakatifu Lulembela jimboni humo .

“Katika safari yetu ya imani Mungu yupo kati yetu, kwa hiyo  waumini  tunapaswa  kufungua  mioyo yetu  ili aweze  kutukirimia mambo makuu katika matendo  ya  wokovu  na  ukombozi wetu hasa wakati huu  tunapoelekea  kumpokea  Masiha Mkombozi wetu,” ameeleza.

Askofu Minde alisema Parokia Teule ya Utatu Mtakatifu , Lulembela  aliyoizindua ni moja ya  matunda ya Yubilee ya Mwaka  wa Huruma ya Mungu   jimboni humo  kwa kuwasogezea karibu waamini huduma ya kiroho na kichungaji  .

Alisema kuwa Parokia ya Utatu Mtakatifu ,  Lulembela ina  kilomita za mlaba 112  , senta 3 vigango  15  na  jumla ya waumini 2069  na imemegwa toka Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Ushirombo na kuwataka  waamini hao kubadilika na  kuachana na maisha ya zamani  na kutimiza wajibu wao  kama parokia.


Ikumbukwe kuwa, hadi sasa jimbo la Kahama  lina jumla ya parokia 23.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU