PUMZIKA SALAMA PADRI ANDREW LUPONDYA




Maaskofu wa majimbo manne , mapadri , watawa na mamia ya waamini  wameshiriki misa ya mazishi ya Padri Andrew  Lupondya (33)  na watoto watano wa  shirika rafiki wa utoto wa Yesu (VIFRA)  na mlezi wao Mama Judith  Kajwahula (63 )  wa jimbo Katoliki Kahama waliofariki  katika ajali ya gari.

Ajali hiyo ilitokana na gari walilokuwemo kugongana uso kwa uso na roli aina ya fuso Disemba 24  na marehemu wamezikwa katika eneo la kiwanja cha  kanisa kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga parokia ya Kahama mjini.

Misa ya mazishi  imefanyika katika kanisa kuu la jimbo na  imeongozwa na Askofu Fravian Kasala wa jimbo Katoliki Geita, pamoja  na  Maaskofu  Liberatus  Sangu wa Shinyanga, Joseph Mlola wa Kigoma  na mwenyeji Askofu Ludovick Minde wa Kahama.







Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU