“Mpelekeni Yesu katika mazingira ya shule”


KUMPELEKA Yesu katika mazingira ya shuleni iwe ni sehemu ya maisha yenu ya kila siku ili kupitia ninyi wanafunzi wezenu wamuone Yesu.
Jinsi mnavyovaa, mnavyoshirikiana, mnavyofwata sheria za shule, mnavyofanya ibada na mnavyosoma kwa bidii. Kuwavute vijana wengine na kuwa na matamanio ya kuishi kama ninyi. Huko ndiko kumhubiri Kristo katika mazingira yenu.”
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Padri Raymond Saba wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa (TYCS) uliofanyika Kurasini, Jijini Dar es salaam.
Padri Saba amesisitiza vijana kuwa wanatakiwa kujituma kutafuta ufumbuzi wa matatizo inayowazunguka ili muweza kuyatatua.


Msali rozari kila siku sio mnazivaa tu hizo rozari na kutembea nazo kwani kuvaa bila kusali ni sawa na hirizi. Msimtafute Mama Bikira Maria kipindi cha matatizo tu bali msali rozari kila siku hivyo ndivyo Mama Bikira Maria alivyotutaka tufanye.
TYCS mnatakiwa kujiendesha wenyewe kwani bado mnayonafasi angalieni namna gani mnaweza kujiendesha bila kutegemea wafadhili .
Ningependa siku moja kuwaona mkiwa viongozi wakubwa katika nchi hii, wakubwa kwa namna ya kuwatumikia watu vizuri kwa haki na usawa kwa kufuata sharia,” amesema Padri Saba.
Pia aliwashukuru walezi kwani wametoa muda wao kuwasindikiza vijana katika mkutano wao wa kufanya uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi pia kuwalea kwenye maadili mema huku akiwasisitiza walezi wengine wawalee vijana vizuri katika malezi ya kila siku.

Mratibu wa vijana Taifa Padri Liberatus Kadio ametoa shukrani kwa viongozi na walezi waliofika kwenye mkutano huo wa uchaguzi wa mwaka. Pia amewapongeza viongozi waliomaliza muda wao wa uongozi akisisitiza kuwa, bado wanahitajika kiutendaji mpaka kongamano la vijana litakapomalizika mwakani.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU