Posts

Showing posts from November, 2019

Askofu Rweyongeza: Wakatoliki msidanganywe na watenda miujiza

Image
WAkristo wakatoliki wametakiwa kuwa na msimamo wa imani na kufuata kanuni na misingi ya Imani ya Kanisa Katoliki. Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo Katoliki Kayanga Mhashamu Almachius Vicent Rweyongeza katika misa Takatifu ya Kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 10 ya Jimbo la Kayanga na miaka 10 ya Uaskofu wake. Misa   hiyo iliyoambatana na uzinduzi wa nyumba ya Kiaskofu Jimboni Kayanga. Amesema kuwa mkristo mkatoliki kamwe hatakiwi kuwafuata wanaokuja   kuwadanganya   na kuwalaghai kwa fedha, magari na mali za kupita hapa duniani . Mkristo anatakiwa kuwa na subira , uvumilivu pamoja na   kuwa na imani thabiti ambayo itasaidia kung’oa visiki na milima na kufuata kanuni msingi za Kanisa Katoliki. Akofu Rweyongeza amesema kuwa ‘’Wahubiri feki huwahubiria watu tusiowafahamu,na wale wenye magonjwa sugu ambao tunawafahamu hawawafuati kuwaponya. Wanatuletea watu feki ambao wameandaliwa   nanyi mnawafuata. wangekuwa waponyaji kweli wangeenda kuponya kw

TEC yatoa mafunzo kwa wanawake kuhusu uchumi shirikishi

Image
BAraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC limetoa mafunzo ya siku mbili kwa wanawake   wa kada mbalimbali juu ya uchumi wa soko jamii. Mafunzo hayo yamefanyika kuanzia Novemba   15 -16 mwaka huu katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Kurasini jijini Dar es Salaamna kuhudhuriwa na wanawake kutoka majimbo zaidi ya 20 kwa maendeleo endelevu na shirikishi y akiuchumi na kijamii. Akifungua mafunzo hayo   Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha Mhasham Prosper Lyimo amewataka wanawake nchini kuitumia vizuri fursa ya mafunzo ya uchumi wa soko jamii shirikishi wanayoyapata ili yawasaidie wao na wengine kujikwamua kiuchumi na kukuza uchumi wa Taifa. Askofu Lyimo amesema Kanisa lina miradi mingi yenye lengo la kuwasaidia watu wote kwa pamoja wa mjini na vijijini, hivyo amewataka wanawake hao kuyatumia vyema mafunzo wanayoyapata kwa manufaa yao na ya wengine sambamba na kutumia karama walizopewa na Mungu kwa manufaa ya Taifa la Mungu kiujumla. Amewapongeza wanawake kwa mwitik

Wanaohitimu elimu ya juu watakiwa kutatua changamoto za wananchi

Image
ASkofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu   Katoliki Tabora amewaasa wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Mihayo Tabora, (AMUCTA) kutumia elimu waliyoipata katika kutatua matatizo ya wananchi wa Mkoa wa Tabora na Tanzania nzima. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni katika Adhimisho la Misa Takatifu iliyoadhimishwa katika Kanisa la Chuo hicho   ambapo Askofu amesema elimu ina lengo la kumsaidia mwanadamu amudu   mazingira yake . Elimu ni ufunguo, elimu ni mwanga unaomsaidia mwanadamu kuwa mstaarabu na kupeleka ustaarabu huo kwa wengine katika jamii anayokuwemo na si kitu cha kumpatia mwanadamu kiburi na majivuno. Askofu Ruzoka amesema, elimu inamsaidia mwanadamu kuwa bora zaidi katika kueleza mambo kwa ufasaha zaidi kwani anakuwa na ufahamu mkubwa zaidi tofauti na hapo awali, elimu hiyo inaongeza ufanisi katika utendaji wake wa kila siku. Amewataka wahitimu hao kumtanguliza Mungu zaidi ili waweze kutafuta Hekima katika Ukweli, “seek Wisdom in truth” ambayo ndiyo kauli m