Posts

Showing posts from March, 2017

MSIBA MZITO: TEC yaomboleza

Image
BAraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC limepata pigo baada ya kuondokewa na Mkuu wa Idara ya Uchungaji Padri Galus Marandu wa Shirika la Roho Mtakatifu(C.SS.P) aliyefariki dunia Jumapili tarehe 26 Machi 2017 Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Katika Ibada ya Misa Takatifu ya kumuaga Padri Marandu iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili TEC, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema Kanisa Katoliki nchini limepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mtendaji mahiri na mwajibikaji mwenye ubunifu katika kuhudumia jamii. “Katika uhai wake, Padri Marandu alikuwa mchapa kazi na alifanya kazi kwa umakini na ufanisi mkubwa. Kipindi cha miaka 15 aliyofanya kazi TEC, Padri Marandu ameacha matunda   yanayoonekana wazi na jamii inajivunia hasa kwa kuhakikisha anawajenga watu katika upendo,   amani, umoja na mshikamano kwa kuwaunganisha watu wa Dini mbalimbali kuwa kitu kimoja kwani jambo hilo si la mchezo na kwa mtu mw

Dada wadogo wa Yesu wameacha utume Afghanstan

BAADA ya miaka 60 ya huduma kwa wahitaji , Shirika la Dada wadogo wa Yesu    limelazimika kuacha kutoa huduma katika   mji wa Kabul Afghanstan    na kulazimika kufunga nyumba zao kutokana na ukosefu wa miito. Hayo yameelezwa na Padri Giuseppe Moretti ambaye amefanya utume kwa muda wa miaka 18 mji Mkuu   Kabul kama msimamizi wa Kanisa lao dogo. Padri huyo amekuwa kwa muda mrefu na hakuacha mji mkuu wakati wa kuingiliwa na   jeshi la Kisovietiki na hata kwa wanajeshi wa kitaleban au wakati wa mabomu ya hapa na pale. Akitoa ushuhuda juu ya historia ya watawa hawa anasema; kuwa kipigo na mateso ya namna hii yamewafanya watawa hawa kuishi na watu karibu, hata walipofika wanajeshi wa Nato mwaka 2000 kutaka kuwahoji watawa hawa hawakupendelea kutoa habari zozote kuhusu watu wao walio kuwa wakiishi nao. Hiyo siyo kwa sababu ya kuogopa ya kwamba wataonekana kama wapelelezi bali ndiyo ilikuwa mtindo na karama yao ya kuhudumia watu kwa ukimya katika mateso. Watu wengi walifika kwa wata

VILIO VYATAWALA MAZIKO YA MAPADRI WATATU NA SISTA JIMBO KATOLIKI MBEYA

Image
askofu wa Jimbo Katoliki Mpanda Mhashamu Gervas Nyaisonga amewataka waamini kumshukuru Mungu kwa   msiba wa mapadri watatu na mtawa mmoja wote wa Jimbo Katoliki Mbeya huku akiwataka wafahamu kwamba vifo ni kielelezo cha maisha ya duniani   kwa waliobaki. Akizungumza katika mahubiri   ya ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa Kuu Jimbo Katoliki Mbeya iliyoongozwa na   Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea Mhashamu Damian Dalu, Askofu Nyaisonga   amesema   kuwa waamini hawana budi kufurahia safari ya mwisho ya    mapadri hao na sista kwa kuzingatia ujumbe wa Baba Mtakatifu Fransisko alioutoa wakati wa Kwaresima na kwamba kila mmoja anawajibika kutekeleza mema kutokana na karama aliyopewa na Mwenyezi Mungu. Kwa upande wake Askofu Anthony Banzi wa Jimbo Katoliki Tanga amemshukuru Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo Katoliki Mbeya kwa kumlea marehemu Padri John Mahundi hadi mauti yalipomfika na akatumia nafasi hiyo kutoa pole kwa   Askofu Chengula na wana Mbeya. KIONG