“Bila uwajibikaji na uwazi Kanisa litakosa miradi”
MAKATIBU wa Idara ya Uchungaji na
Mawasiliano wameaswa kuwa mawakala sahihi wa utawala wa rasilimali, uwajibikaji
na uwazi katika utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na wafadhili ili kusaidia
shughuli mbalimbali Kanisa.
Hayo yamesisitizwa na Naibu Katibu Mkuu
wa AMECEA, Padri Chrisantus Ndaga wakati wa warsha juu uratibu madhubuti wa
rasilimali fedha na watu kwa Makatibu wa Idara ya Uchungaji na Mawasiliano
pamoja na baadhi ya wanachama kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika
Mashariki (CUEA) na baadhi ya wahabari watendaji kutoka nchi wanachama wa AMECEA
Padri Ndaga amewasisitiza washiriki kuwa makini na ubunifu ili kusaidia
ofisi zao na mabaraza yao kwa lengo la kuwa na maendeleo endelevu.
“Lengo la warsha hii ni kutoa ujuzi kwa Waratibu wa kichungaji,
Mawasiliano na wanahabari wetu ambao wanahusika moja kwa moja katika kuendeleza
ofisi za mawasiliano na Kichungaji ili wapate elimu juu ya uhamasishaji wa
rasilimali fedha na kuanzisha uhusiano mzuri na washirika ili kutoa huduma bora
kwa Kanisa.
Katika mahojiano maalum, na mwezeshaji
wa semina Hillary Korir, ambaye ni Mkurugenzi wa Caritas Jimbo Katoliki Nakuru
Kenya amesema semina ni wakati muafaka kwa sababu umeleta pamoja waratibu wa
Uchungaji na Mawasiliano ambao kwa kweli wanahitaji elimu ya utawala na
kumudu rasilimali ili kuboresha ujuzi
wao na kupata maarifa juu ya kuandika miradi na ripoti zinazokidhi vigezo vya
wafadhili na Kanisa kwa ujumla.
"Hapo awali ilikuwa ni rahisi
kupata fedha za wafadhili kuendesha shughuli za Kanisa. Ungeweza kuandika
karatasi moja ukapata fedha. Lakini leo hii unapaswa kuandikamambo mengi
kwakutii vigezo vya wafadhili kwani wanaoomba msaada ni wengi kuliko wanaotoa.
Siku hizi mambo yamebadilika mahitaji ni ya watu wengi, ushindani ni mkubwa na
si rahisi kupata fedha tena, "amesema.
Katika mada yake, mwezeshaji
alibainisha kuwa miradi mingi hukataliwa na na wafadhili kutokana na sababu
kadhaa ikiwa ni pamoja na kuandika matatizo yasiyoeleweka, miradi isiyo na
vigezo katika mahitaji fulani, kushindwa
kuandika ripoti kwa wakati, , ukosefu wa uwajibikaji na kukosa ujuzi wa kuandaa
miradi.
“Zamani waliokuwa wanaandikamiradi
walikuwa ni wataalamu wa miradi lakini dunia imebadilika kila mmoja katika
ofisi yake iwe ni ya uandishi wa habari, elimu, liturujia, afya nk. Kila mtu
anapaswa kuwa na utaalamu wa kuandika mradi ili kukidhi mahitaji ya Kanisa na
ofisi husika. Hivyo wanamawasiliano hii ni fursa ya kuleta maendeleo chanya
katika kujitegemeza na kuinjilisha kwa kina. Kinachotakiwa ni kuwa wabunifu wa
miradi,” amesisitiza.
Washiriki walikuwa changamoto kwa
kujifunza na kuwa na sanaa ya kuendeleza mapendekezo, kuhusisha washauri ikiwa
ni lazima, kuendeleza mapendekezo kwamba kushughulikia mahitaji maalum ya jamii
na wakati huo huo, kujitahidi kuunganisha mipango kwa manufaa ya jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Mawasiliano Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya Bw. David Omoyo amesisitiza kuwa
katika kila ofisi ya Baraza la Maaskofu lazima kila mmoja achangamkie fursa za
kuandika miradi wakati anaangalia zipi changamoto, fursa, udhaifu na vitisho
vya miradi anayoiandika.
“Unaweza kuandika mradi yako ukauona ni
bunifu wenye utaalamu wa hali ya juu kumbe kuna wengine zaidi ya 3000
wameandika miradi kama yako kwa kuwa matatizo ya Kanisa wakati mwingine ni
yaleyale. Hivyo ukiwa mbabaishaji katika kuandika hususani matokeo ya mradi
mzima pia changamoto hutapata na wala hawatasoma. Hivyo ujuzi wa hali ya juu
unatakiwa,” amesisitiza.
Ameshauri kila mmoja katika ofisi za
mabaraza ya Maaskofu Katoliki nchi za AMECEA kuwa na ubunifu wa kutaka
kujiendeleza kwa kuandika miradi mbalimbali badala ya kutegemea mtu maalumu wa
kuandika mradi.
“Mtu
maalumu anaweza kuwepo lakini mara nyingi anachelewesha mambo kwani anakuwa na
shughuli mbalimbali. Ni vyema kila mmoja akajifunza ili kurahisisha kazi na
kuleta ufanisi zaidi.”
Comments
Post a Comment