KONGAMANO LA EKARISTI TAKATIFU 2020 KUFANYIKA JIMBO KUU TABORA
MAaskofu, mapadri na waamini wa majimbo Katoliki
Kanda Ya Magharibi wameanza maandalizi rasmi ya kuwa wenyeji wa Kongamano la
Ekaristi Takatifu kitaifa mwaka 2020.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku moja cha maandalizi hayo
Jimboni Tabora, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka
amewaomba wana Kanda ya Magharibi kumshukuru Mungu kwa kupewa heshima kubwa na
Kanisa la Tanzania kwa kuwa wenyeji wa Kongamano hilo kitaifa hivyo ni vema
washirikiane katika kufanikisha kazi hiyo ya Mungu.
Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na majimbo
yanayounda Kanda hiyo ya Magharibi kukusudia kuandika kitabu kitakachotoa
historia nzima ya Ukristo ndani ya majimbo hayo. Pamoja na historia hiyo pia
historia ya Ukristo toka mlango wa Imani Bagamoyo nayo pia itaandikwa.
Akizungumza na Gazeti hili Askofu Mkuu Ruzoka amesema majimbo yote
yanaandaa utaratibu wa kupata wawezeshaji wa Mada mbalimbali zitakazotolewa juu
ya Ekaristi Takatifu ili kuongeza uelewa kwa washiriki watakaoshiriki katika
kongamano hilo.
Inakadiriwa washiriki wa kongamano hilo watakuwa 6,700 na gharama ya kila
mshiriki itatolewa baada ya gharama halisi kuwa imebainishwa na kamati ya
inayoratibu gharama za kila mshiriki na kutumwa hapo baadaye ili kila mtu
anayependa kushiriki aanze maandalizi mapema.
Maaskofu walioshiriki mkutano huo ni:
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka, Askofu
wa Jimbo Katoliki Kahama Mhashamu Ludovick Minde na Askofu wa Jimbo Katoliki
Kigoma Mhashamu Joseph Mlola.
Kongamano hilo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 30 Juni 2020 Jimboni
Tabora.
Comments
Post a Comment