MADAKTARI WATANZANIA WAENDELEA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA 500 KENYA
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu
amewashauri madaktari wa Tanzania ambao hawana ajira za serikali na
wanakidhi vigezo waendelee kuomba nafasi za ajira nchini Kenya, huku
akitaja idadi ya waliokwishaomba.
Kutpitia
mtandao wake wa twitter, Waziri Ummy amesema hadi sasa ndani ya siku
moja pekee, tayari kuna madaktari zaidi ya 150 tayari wamekwishaomba
nafasi hizo.
"Sisi
tunaendelea kupokea Maombi. So far, kwa siku ya 1 tu tumeshapokea zaidi
ya 150! Naendelea kutoa Wito kwa MDs wetu kutoiacha fursa hii."
Ameandika Waziri Ummy Mwalimu.
Amesema mwisho wa kutuma maombi hayo ni tarehe 27 Machi, 2017.
Serikali
ya Tanzania hivi karibuni ilikubali kuwapeleka madktari wake 500 nchini
Kenya, kutokana na mgogoro unaoendelea nchini humo, uamuzi ambao
umepingwa na vyama vya madaktari vya nchi zote mbili yaani Tanzania na
Kenya.
Kwa
mujibu wa taarifa aliyoitoa Waziri huyo, alisema kwa sasa Tanzania
haina tatizo la madaktari, bali kuna changamoto ya kuwaajiri madaktari
waliopo.
"Katika
kipindi cha mwaka 2013/14 hadi 2016/17 madaktari 2,439 wamehitimu. Kati
ya hao serikali imeajiri 615 tu. Pia watakaoajiriwa mwaka 2017/18
hawatazidi 600 ..... Hivi sasa hatuna tatizo la uwepo wa madaktari.
Changamoto yetu ni kuwaajiri tunaozalisha" Alisema Ummy
Alisema Tanzania kwa sasa ina uwezo kuzalisha takribani madaktari 1,200 kwa mwaka."
Comments
Post a Comment