Kanisa lajitosa kunusuru uharibifu wa mazingira Mlima Wotta
VIONGOZI wa
Kanisa Katoliki Parokia
ya Kibakwe, Jimbo
Kuu Katoliki Dodoma,
wamesema kuwa endapo
serikali haitazuia uharibifu wa
mazingira katika Milima
ya Wotta ambayo
ndiyo chanzo cha
maji kwa vijiji takribani 10 vya wilaya
hiyo, wilaya hiyo huenda
ikakumbwa na uhaba mkubwa
wa maji na ukame.
Viongozi hao wakiongozwa na
Padri Selestine Lipambile na
viongozi wengine waliotoka
vigango vya Lukole
na Kingiti wametembelea milima hiyo ili kuangalia uwezekano
wa Kanisa kusaidia
upatikanaji wa maji
ya uhakika toka
vyanzo vya maji
ya vijiji hivyo.
Katika tathmini yao wamebain kuwa
uharibifu wa mazingira
katika vyanzo hivyo
ndiyo chanzo kikuu cha uhaba wa maji ulioanza kukumba wakazi wa maeneo
hayo kitu ambacho serikali
wilayani humo wameshindwa
kuzuia .
Wakitoa
mfano wa uharibifu mkubwa
ulifanyika katika mlima
wa viongozi hao wamejionea
eneo hilo likiwa limeharibiwa kwa
kugeuzwa eneo la
mashamba huku kukiwa
na chanzo hicho
kikuu cha maji
cha vijiji hivyo . Wamesema kuwa
ni jambo la
ajabu serikali imekaa
kimya wakati watu
wanaendelea kuteseka kwa
kukosa maji ya
uhakika.
Akiongelea tatizo
hilo Padri Lipambile amesema kuwa
kutokana na shughuli za kilimo kufanyika katika vyanzo
vya maji, hali hiyo imesababisha mchanga
kujaa katika chanzo
hicho kwa sababu
hakuna miti na
kuwafanya wananchi wa
kata nzima ya
Kingiti kukosa maji
kwa miaka mingi.
Padri
Lipambile ameongeza kuwa
viongozi wa eneo
hilo wameliomba kanisa
kuangalia uwezekano wa
kusaidia upatikanaji wa
maji eneo hilo lakini
kutokana na kukithiri kwa shughuli za
kilimo cha ovyo
katika chanzo hicho
na vyanzo vingine
kanisa halioni haja
ya kusaidia kwani
msaada huo utakuwa
kazi bure kama
kilimo na uharibifu
huo utaendelea bila
serikali kuchukua hatua
kali dhidi ya
waharibifu hao .
“Ulegevu wa viongozi wetu hapa
ndiyo uliotufikisha hapa
tulipo, kwa sababu
ya kulinda maslahi ya mtoto
wa mjomba au
mtoto wa shangazi” amesema .
Comments
Post a Comment