Dada wadogo wa Yesu wameacha utume Afghanstan
BAADA ya miaka 60 ya huduma kwa wahitaji , Shirika
la Dada wadogo wa Yesu limelazimika
kuacha kutoa huduma katika mji wa Kabul
Afghanstan na kulazimika kufunga nyumba
zao kutokana na ukosefu wa miito.
Hayo yameelezwa na Padri Giuseppe Moretti ambaye
amefanya utume kwa muda wa miaka 18 mji Mkuu
Kabul kama msimamizi wa Kanisa lao dogo.
Padri huyo amekuwa kwa muda mrefu na hakuacha mji
mkuu wakati wa kuingiliwa na jeshi la
Kisovietiki na hata kwa wanajeshi wa kitaleban au wakati wa mabomu ya hapa na
pale.
Akitoa ushuhuda juu ya historia ya watawa hawa
anasema; kuwa kipigo na mateso ya namna hii yamewafanya watawa hawa kuishi na
watu karibu, hata walipofika wanajeshi wa Nato mwaka 2000 kutaka kuwahoji watawa
hawa hawakupendelea kutoa habari zozote kuhusu watu wao walio kuwa wakiishi
nao.
Hiyo siyo kwa sababu ya kuogopa ya kwamba
wataonekana kama wapelelezi bali ndiyo ilikuwa mtindo na karama yao ya
kuhudumia watu kwa ukimya katika mateso.
Watu wengi walifika kwa watawa kuomba msaada,waliwasikiliza kwa upendo
historia zao na zilibaki ndani ya mioyo yao.
Ili kuweza kushirikiana na wakazi hao,watawa hawa
waliweza kuongea lugha ya wenyeji ili kushiriki bege kwa bega na watu rahisi na
masikini , kwa njia hiyo watawa walipendwa na kusifiwa na jumuiya nzima ya watu
kiasi kwamba miaka ya hivi karibuni
walikuwa wametunikiwa uraia wa Afghanstan.
Watawa wa Dada wadogo wa Yesu waliheshimiwa sana
hata na maaskali wa Waktalebani.
Anakumbuka kwamba mwaka 1993 wakati wa vita, Ijumaa wote walikuwa wanakwenda hata katika
kikanisa cha Ubalozi kusali, japokuwa Kikanisa hicho kilikuwa imefungwa kwa
sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Watalebani waliwatambua ni wakina nani
na hivyo waliaacha waingie kusali.
Mbele ya Kikanisa hicho kuna msalaba mkubwa
unaoonekana. Nyumba ya watawa hao
ilikuwa karibu na sehemu ya ubalozi, kwa njia hiyo wangeweza hata kuharibu
Kanisa hilo lakini hawakufanya hivyo. Ijapokuwa mtawa wa mwisho kuondoka ilikuwa
ni mwezi Februari 2017, historia yao ni muhimu kabisa katika nchi hii ya
Afghanistan, Padri Moretti anaongeza.
Hawa ni watawa walioitikia wito kujibu upendo
wa Mungu
na kumfuasa Kristo katika kuiishi Injili .
Ni roho iliyojikita katika ukimya wa kujitoa, sala , urafiki na matendo kwa kukumbatia
ulimwengu.
Shirika hili lilianzishwa na Mgdaleine wa Yesu kwa
ushirikiano na Mwenyeheri Charles de Foucauld maarufu kama Padri wa kiroho
aliyeishi katika maeneo ya jangwa.
Mwenyeheri Charles de F. anakumbukwa sana na wosia
mwingi wa kiroho katika maisha ya waamini kila siku kwani ni kutokana na uzoefu
wake kabla ya kumtambua Mungu ni nani kwake, nawakati anajitafakari maisha yake
aliandika maneno kwa kumwelekea Mungu akisema “Kama upo ee Mungu nipe neema ya
kukutambua” lakini baada ya kumjua ya kwamba Mungu yupo akasema “Asingeweza kufanya lolota zaidi ya kuwa naye
mpaka milele” (1901). Kwa njia hiyo watawa wa kike na kiume wamefuata nyayo zao
za Yesu wa Nazareth kwa kutoa huduma yao
pande zote za dunia.
Upendo wa Yesu Mwenyeheri Charles de F. ulisababisha
yeye kuwa ndugu wa wote bila ubaguzi na ameandika kwamba “utume wangu unapaswa
uwe wa wema. Kwasababu atakaye niona lazima asema kwakuwa mtu huyu ni mwema na
hivyo dini yake lazima ni nzuri.”
Vilevile anasema
“Kama nikiulizwa kwani mimi ni mpole na mwema, lazima kusema kwasababu
mimi ni mtumishi wa mtu aliye mzuri zaidi ya mimi”.
Anaongeza ,
”Kama tungelijua jinsi gani Bwana Yesu ni mwema,… ninatamani niwe mwema zaidi
hadi wasema , kama mtumishi huyo ni mwema hivyo , Je Bwana wake yuko je?”.
Mwanzilishi Mkuu wa Shirika Charles de Foucauld
akiwa na Mgdaleine wa Yesu ameandika tafakari nyingi sana za kiroho kuonesha
upendo mkubwa wa Yesu alio kuwa nao ambazo ni urithi kwa waamini wengi , pamoja
na kwamba ndiyo mwongozo wa dada wadogo wa Yesu ambao kwa miaka 60 wameweza
kufanya huduma ya kitumea katika nchi ya Afghanstan na sasa wameng’atuka
kwasababu ya kukosefu wa miito katika eneo hilo.
Comments
Post a Comment