PAPA KUZURU AFRIKA APRILI


Dr. Greg Burke msemaji mkuu wa Vatican amesema, Baba Mtakatifu Fransisko amekubali mwaliko uliotolewa na Rais wa Misri, Baraza la Maaskofu Katoliki Misri , Mheshimiwa Sana Papa Tawadros II pamoja na Sheikh Ahmed Mohamed El Tayyib wa Msikiti Mkuu wa Al Azhar, mjini Cairo, ili kutembelea Misri kuanzia tarehe 28- 29 Aprili 2017. Kwa namna ya pekee kabisa, Baba Mtakatifu Francisko atatembelea mji wa Kairo. Taarifa zinabainisha kwamba, wakati wowote kuanzia sasa ratiba elekezi ya ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Barani Afrika itatolewa na Vatican.
  
VATICAN

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU