TUTUMIE KWARESIMA KUSAIDIA WAHITAJI- KAMANDA WA JESHI LA POLISI RUKWA
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa polisi
George Simba Kyando amewataka watanzania kutumia vema kipindi hiki cha Kwaresima
kwa kuachana na dhambi na badala yake kuwasaidia wahitaji mbalimbali katika
jamii.
Akikabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali kwa watoto yatima
katika kituo cha malezi cha mt. Martin de porres kilichopo katandala
kinachomilikiwa na shirika la masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika
MMMMMA Jimboni sumbawanga kwa niaba ya
jeshi la polisi mkoani Rukwa kamanda kyando amesema kuwa ni vema jamii
ikatambua uhitaji wa vituo vya watoto yatima kwa kusaidia huduma na mahitaji
kwa watoto pasipo kujali nafasi za kazi,vyeo,madaraka,hali za maisha dini au
siasa kwani wlelewa si wa dini wala kabila
Hatua hii imekuja ambapo jeshi la polisi mkoani rukwa
linaadhimisha wiki ya kipolisi mkoa na kwa kipindi hiki cha kwaresima limeona
ni vema kutoa mchango kwa watoto yatima.
Akipokea mchamgo huo kutoka jeshi la polisi mama mkuu mlezi
wa kituo hicho Sister Scholastika Wampembe amelishukuru jeshi la polisi mkoa wa
Rukwa kwa kujali na kuguswa na maisha ya watoto yatima na kutoa wito kwa jamii wananchi,serikali,
mashirika ya dini na makampuni binafsi kuendelea kusaidia kwani ni changamoto
nyingi zinazowakabili katika malezi ya watoto hao ambapo kwa sasa kina jumla ya
watoto 31.
Kituo cha Mt. Martin de pores kilianzishwa mwaka 1963 katika
parokia ya mwazye na baadae kuhamishiwa manispaa ya Sumbawanga mnamo mwaka 1974
kwaajili ya kuboresha huduma zake ambapo kinapokea watoto kutoka sehemu
mbalimbali ndani ya nchi bila kujali dini,rangi,kabila na Taifa.
Kituo hiki kilianzishwa kwa malengo ya kuwatunza watoto
wanaofiwa na mama zao baada ya kuzaliwa, kutunza watoto wanaotelekezwa na mama
zao wakiwa wachanga na watoto ambao wazazi wao wana ulemavu wa akili.
Kituo cha kulelea watoto yatima cha martn de pores
kinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa mishahara ya
wafanyakazi, huduma za umeme,maji,dawa na huduma zingine za kimalezi kwa watoto
yatima
Na Emmanuel Mayunga, Rukwa
Comments
Post a Comment