Kard. Pengo ahimiza Watoto wafundishwe kuwa wamisionari wazalendo

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amehimiza wazazi, jumuiya na Kanisa kwa ujumla kuwafundisha watoto kuwa wamisionari wazalendo ili baadaye jamii ipate kizazi kinachoweza kuwajali wengine.
Kardinali Pengo amesema hayo hivi karibuni alipoungana na Watoto wa  Shirika la Kimisionari la Utoto Mtakatifu Jimbo Kuu Dar es Salaam wa Dekania ya Ubungo na Kibaha  walipowatembelea watoto yatima na wazee wanaolelewa katika nyumba zao zilizopo Msimbazi  senta Dar es Salaam.
“Wamisionari si wenye pesa tu, wamisionari hawatoki Ulaya. Mawazo hayo nadhani yameshatoka katika mioyo ya waamini wetu hususani wa Dar es Salaam. Mmisionari ni mimi wewe si lazima atoke ulaya. Kutoa msaada kwa wazee na watoto yatima ni  kuonesha umisionari kati yetu.
Tunafahamu kuwa watoto hawana kipato chochote lakini wanaweza kuwasaidia wengine kupitia wazazi wao. Tunawalea katikamazingira ya kuona utu wa mwanadamu, thamani ya wanadamu wengine hususani wenye shida. Wakiwa watu wazima watakuwa wanakumbuka na tayari tumeshawaandaa kuwa na huruma kwa wenye shida. Hii ndiyo dhana ya kuwapeleka kufanya matendo ya huruma kwa wenye shida mbalimbali. Tunalea kizazi kinachojali wengine,” ameeleza Kardinali Pengo huku akisisitiza;

Leo ni siku ya kufanya matendo ya huruma kwa wenye shida hususani katika kipindi hiki cha majilio. Wale wenye dhiki na shida sisi Utoto Mtakatifu tunajitahidi kufanya matendo ya huruma kwa wazee wasiojiweza, watoto wasio na wazazi.
 Wote sisi wana utoto mtakatifu tunajihusisha nao kwa lengo kubwa kwamba tunakua kwa pamoja kwa mawazo ya huruma na upendo.
Watot wakizoea kufanya hivi wakiwawakubwa watasaidia wengne wenye mahitaji.
Maneno waacheni watoto wadogo waje kwangu, ni maneno ya Kristo. Alipenda sana watoto wadogo. Anatukumbusha upendo wa Kristo kwa watoto, watoto wajisikie wamefika kwa Kristo mwenyewe.
Mara kwa mara watoto wa utoto mtakatifu wanafanya matend ya huruma. Lengo letu kubwa ni kuandaa wamisionari wa leo na siku za mbele katika taifa letu kwa moyo uleule waliokuwa nao.

Tunapokuja mahali kama hapa hususani kwenye kipindi cha maajilio, kuwahudumia hawa watoto ni kwamba tungekuwepo Bethlehem tusingemuacha mtoto Yesu akazaliwa pangoni. Tungempa nafasi nzuri. Sisi tunamhudumia Kristo kupitia watoto hawa wadogo waliozaliwa wazazi wakafariki ama wakawatelekeza.”

Akizungumzia juu ya watoto waliotelekezwa na wazazi wao, Kardinali Pengo amesema kuwa,Kwa destiri watoto walotelekezwa ni ishara inayotia uchungu. Mtua anazaa mtoto halafu anamtelekeza. Hata kama hana uwezo ina maana hana ndugu au jamaa. Watoto pengine baba hajulikani mama anaona ugumu wa kumlea peke yake.
“Kweli mtoto wa kike anaweza kuzaa mtoto tukashindwa kumlea? Hata kama si wa kabila letu, rangi yetu na hatujui baba ni nani lakini tunao wajibu wa kuwalea watoto hawa ili wasitelekezwe ama kuuawa.
Ni wazi kuna wanaopata watoto katika mazingira yasiyoeleweka. Tuna wajibu wa kuwalea na kuwasaidia. Ndiyo maana ninasisitiza kuwa lazima kila mtu walau awe na jumuiya yake, akiwa ana matatizo jumuiya haipaswi kumtupa nje, imsahihishe asiharibike.
Wengine wanawaua, kuwatupa kwenye maji machafu, mazingira mabaya nk. Haya yanatokea kwa mabinti wetu. Lazima  tuwakemee kwa yale wanayofanya lakini tuwajengee mazingira ya kujiepusha na hatari hizo.
Ndiyo maana Kanisa linawalea watoto wa Utoto Mtakatifu ili wakue katika maadili ya Kikristo,” ameeleza.
Amewahimiza wale wanaowalea watoto hao yatima kuwa wanapaswa kusimamia na kuwalea watoto katika maadili na wajitoe kwa moyo wote.
“Waacheni watoto wadogo…. Hawa wanasimama badala ya kristo mwenyewe.
Kristo hakuwafukuza, aliwakumbatia na kuwabariki. Kupitia wao, watoto wajisiskie wanapendwa na Kristo.
Aidha amewahimiza waamini kujitoa kuwalea watoto na wazee kwani ni jukumu lao. Wasiiache serikali na  Kanisa.
Kwa upande wake mzee Peter Matimbwa (78) amemshukuru Kardinali Pengo pamoja na watoto wa Utoto Mtakatifu kwa zawadi walizowapatia nakusali pamoja nao.

Watoto hao walitoa fedha taslimu milioni 2 na vitu mbalimbali vyenye thamani y ash. Milioni 1.338.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU