‘Ukristo ni vita’ Ask. Amani
WAKRISTO wakatoliki
nchini wametakiwa kutambua kuwa ukristo ni vita na mapambano ambapo maisha ya
hapa duniani ni ya muda kwa ajili ya kujiandaa na maisha ya milele.
Rai
hiyo imetolewa na Askofu Mkuu Isaac Amani wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha wakati
akitoa homilia yake kwenye adhimisho la Misa Takatifu ya kilele cha Jubilei ya
miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara kanda ya kaskazini, Misa iliyoambatana
na sherehe ya Bikira Maria mpalizwa mbinguni.
Askofu
Amani amesema kuwa mpango wa Mungu mara zote ni kumuokoa mwanadamu, na maovu
anayoyatenda mwanadamu yanakwenda kinyume na mpango wa Mungu, kwa kuwa Mungu
anashughulikia wokovu kwa sababu binadamu ana thamani mbele yake.
Askofu
Amani amesisitiza kuwa kila mwanadamu hana budi kujitathmini na kujichunguza
kwani mpango wa Mungu siku zote ni wokovu hivyo kila mmoja ana wajibu wa
kujiuliza kama ni wakala wa Mungu ama wa shetani kwa matendo.
Vijana
ni zamu yenu kuwa wamisionari
Wakati
huo huo vijana na watoto wakatoliki nchini wametakiwa kuienzi roho ya
kimisionari, ili siku moja wote wakutane mbinguni.
Wito
huo umetolewa na Askofu Rogath Kimaryo wa Jimbo Katoliki Same wakati akitoa
salamu katika Misa ya Kilele cha miaka 150 ya Ukristo Tanzania Bara kanda ya
Kaskazini.
Askofu
Kimaryo amesema kuwa roho ya kimisionari ni roho ya kanisa na ni asili yake,
hivyo ameomba roho hiyo iwaguse vijana wote wa kike na wa kiume ili wazaliwe
wamisionari wapya.
Katika
hatua nyingine Askofu Kimaryo amewataka mapadri hasa wa majimbo nao kujenga
roho ya kimisionari akisema kuwa lazima mapadri wawapende wamisionari, vijana,
masista ili wazidi kuieneza habari njema ya wokovu kwani hiyo ndiyo furaha ya
injili.
Naye
Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki
Moshi Padri Deogratias Matika ametoa rai kwa waamini kuzingatia sakramenti zote saba walizopewa na
Kristo hasa zile zinazowahusu na kuacha kuutafuta unafuu.
Padri
Matika amesema kuwa kila mmoja akisimama kwa kile alichofundishwa akiwa kama
mklero, muumini mkatoliki na mtawa basi ufalme wa Mbinguni ni juu ya kila
mmoja.
Misa
ya Kilele ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara, kanda ya Kaskazini
imefanyika katika Parokia watakatifu Malaika wakuu Himo, Jimbo Katoliki la
Moshi na imeongozwa na Askofu Mkuu Isaac Amani wa Arusha, Askofu Rogath Kimaryo
wa Same, Askofu Antony Lagwen wa Mbulu na Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki
la Moshi Padri Deogratias Matika.
Comments
Post a Comment