UJUMBE WA PAPA FRANSISKO WA 52 SIKU YA MAWASILIANO DUNIANI 2018
SIKU ya Upashanaji wa habari huadhimishwa kila mwaka katika maadhimisho
ya sherehe za Kupaa Bwana Mbinguni ambapo mwaka huu itafanyika Mei 13. Ujumbe
huu unaongozwa na kauli mbiu “UKweli utawawekeni huru: Habari potofu
(Fake news) na uandishi wa amani”
Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu,
anasema, katika mpango wa Mungu, mawasiliano ya binadamu ni muhimu katika
kuishi umoja. Kama Binadamu ni sura na mfano wa Mungu ana uwezo wa kujieleza na
kushirikishana ukweli, uzuri na wema. Ana uwezo wa kusimulia uzoefu wake
binafsi katika dunia na kujenga kumbukumbu ya uelewa wa matukio.
Lakini binadamu kwa kuongozwa na
ukiburi wake na ubinafsi hawezi kutoa mawasiliano mema kama inavyojionesha katika
matukio ya Biblia katika historia ya Kaini na Abeli, hata tukio la Mnara wa
Babeli. (Mw 4,1-16; 11,1-9).
Kubadilisha ukweli ni dalili ya
kawaida ya upotofu ambayo mtu hufanya binafsi na kwa pamoja. Kinyume chake
katika imani kwa mantiki ya Mungu, mawasiliano ni sehemu ya kuelezea
uwajibikaji kwa kutafuta ukweli na ujenzi wa wema. Leo hii lakini katika dhana
ya mawasiliano, daima inayojionesha wepesi na ndani ya mfumo wa kidigitali,
kwani yanaonekana matukio mengi ya habari za uwongo ziitwazo fake news.
Kulingana na haja hiyo Baba
Mtakatifu anapendelea kutoa ujumbe wa mada ya ukweli ambayo anasema, mara
nyingi watangulizi wake kuanzia mwenye heri Paulo VI (katika ujumbe wa mwaka
1972; ilikukuwa na mada ya “Mawasiliano ya kijamii katika huduma ya ukweli”).
‘Fake news’ ni jambo nyeti
linalojadiliwa na kitu cha mjadala! Kwa ujumla unajikita kutazama kwa kina juu
ya utoaji wa habari za upotofu katika mitandao ‘Online’ au katika mitandao
kijamii, na ya utamaduni asili. Kwa maelezo hayo ni kusema kuwa, ni habari za
uwongo, zisizo na msingi kwa uwepo wake; zenye nia ya kutaka kudanganya hadi
wasomaji na watazamajiwake. Usambazaji wa fake news unaweza kujibu lengo
walilokusudia, kwa kushawishi uchaguzi wa kisiasa na kukuza mapato yao
kiuchumi.
Ufanisi wa fake news
unajitokeza awali ya yote mahali ambapo wao wanaigiza kwa asili yao yaani uwezo
wa kutaka kuonekana na kusifika. Na hatua ya pili, habari za uwongo ambazo
zinafanana, zinavutia, kwa maana ya kupendwa na kuchukuliwa makini na walengwa.
Kwa kuwa na uwezo wao wa kulaghai, hufanya marudio ambayo yanasambaa kwa haraka
ndani ya maisha ya kijamii na kuwatumia wenye hisia rahisi, kuziamsha kwa
haraka, kwa mfano wa kuleta wasiwasi,dharau,hasira na kuchanganyikiwa.
Usambazaji wa habari za
uongo unatumia kwa ujanja mitandao ya kijamii na kwa mantiki ya kuhakikisha
inafanya kazi. Kwa namna hiyo mambo msingi yaliyomo ndani ya habari za uongo,
pamoja na ukosefu wa msingi, unapata mwonekano hadi kufikia mamlaka husika
kukosa uhalifu wake.
Baba Mtakatifu anazidi kufafanua
kuwa, matatizo yanayoonesha kusambaa kwa habari za uongo yametokana
na kwamba watu wengi mara nyingi wako katika mazingira ya kidigitali ya pamoja,
ambayo ni rahisi kupitia mantiki nyingi na maoni tofauti.
Na matokeo ya mantiki ya habari
potofu, ni kwamba, badala ya kukabiliana vema na vyanzo vingine vya habari,
jambo ambalo linaweza kuleta uchanya wa mjadala na kufungua mazungumzo ya
ujenzi, inageuka kuwa hatari hata bila utashi wa wadau wake ambao usambaza
maoni ya uwongo na ushahidi.
Tishio la habari potofu
ni ung’oaji wa mzizi wa mwingine na uwepo wake unakuwa kama adui, hata kuwa
shetani ambaye anaweza kutoa ushahidi wa migogoro ya uwongo; ndivyo
habari za uwongo zinavyjionesha uwepo wake hasa tabia ya kutojali,
anasisitiza Baba Mtakatifu Fransisko.
2.Ni jinsi gani ya
kutambua?: Baba Mtakatifu Fransisko anasema, hakuna hata mmoja
anayeweza kusamehemewa jukumu la kupinga uongo huo! Lakini pia anatambua
kwamba, si kazi rahisi, kwa maana usambazaji wa uwongo unapitia katika
mazungumzo mengi ambayo yanasambaratika kichini chini pia udanganyifu wake
mara nyingi ni wenye mfumo wa kisirisiri.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu
anasistiza kwamba iwapo inawezekana basi kuanzishwa mafundisho ambayo
yanajikita hasa kuchukua hatua ya kusoma na kuchunguza mantiki hiyo ya mawasiliano.
Ni mafundisho ya dhati ili kuweza kuacha tabia ya usambazaji wake; kuwa na
utambuzi kwamba habari zenye uwongo na kwa maana hiyo, kuwa na wadau wa kueleza
wazi wahusika.
Licha ya hatua hiyo ya
mafunzo ni pamoja na ile ya kuanzisha taasisi na kisheria ambazo
zinajikita kwa kina katika kusitisha matukio hayo, kama vile hata taaluma ya
hali ya juu ya kiteknolojia na makampuni ya mitambo ya kutafuta dhana mpya ya
kuhakiki na kuwatambua wahusika wanaojificha nyuma ya milioni ya picha za kidigital.
Hata hivyo Baba Mtakatifu
anabainisha kuwa, uzuiaji na mtambo wa ugunduzi wa habari za uwongo, awali ya
yote unahitaji hata umakini wa kina na mang’amuzi. Ki ukweli ili kuweza
kuwagundua, Baba Mtakatifu anaongeza kuna kile ambacho chaweza
kuelezwa kwamba ni mantiki ya nyoka, mwenye uwezo wa kujificha mahali
popote ili aweze kuuma.
Inahitaji mkakati wa
nyoka mjanja ambaye anatajwa katika Kitabu cha Mwanzo, yeye alikuwa wa kwanza
kumdanganya binadamu ikawa ndiyo fake news ya kwanza (Mw
3,1-15), baadaye ikasababisha majanga yote ya dhambi hadi kufikia mauaji
ya kwanza, Kitabu cha mwanzo sura ya 4, na hata katika idadi kubwa
ya mitindo ya ubaya dhidi ya Mungu, jirani, jamii na kazi ya uumbaji.
Mkakati wa uwezo huyo
aitwaye baba wa uwongo kama Injili ya Yohane ilielezavyo, ( Yh 8,44) ni
mkakati wa kujibuluza,wa hatari ya ulaghai kwani anatengeneza njia katika moyo
wa binadamu kwa kutumia maelezo mengi ya uwongo na kutamanisha. Hayo
yanajionesha katika maelezo ya dhambi ya asili, kwani, mshawishi alimkaribia
mwanamke na kujifanya kama rafiki akionesha kujali wema wake,
akaanza mazungumzo utafikiri ya kweli, lakini yalikuwa ukweli nusu
nusu:“Ni kweli Mungu alisema: mwaweza kula matunda ya mti wowote katika
bustani, lakini matunda ya mti wa ujuzi wa wema na mabaya msile.... (Mw2,17).
Mwanamke alijibu na kuelezea
nyoka, lakini kwa kutaka kumfafanulia zaidi: “Twaweza kula matunda ya mti
wowote bustanini, lakini matunda yaliyoko katikati ya bustani msiuguse ili
tusije tukafa (Mw 3,2)
Baba Mtakatifu anafafanua, Jibu
hili la mwanamke linatolewa kama vile la kisheria na lenye ugumu: kwa
maana alionesha imani kwa mshawishi na kujiachia avutiwe naye, ndiyo maana
mlaghai akabadilisha majibu hayo, akamwambia mwanamke “hamtakufa (Mw 3,4)
“kwa maana alisema hivyo kwasababu anajua kwamba mkila matunda ya mti huo
mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua mema na mabaya”! Mw 3,5).
Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu
anasema, nyoka alikuwa amefanya kazi yake ya kumwondoa mwanamke katika amri ya
Mungu iliyokuwa ya wema na kufuata ushawishi wa adui shetani kwa maana
“mwanamke huyo aliona kuwa mti huo ni mzuri kwa chakula na wavutia macho”… (Mw
3,6).
Baba Mtakatifu anasisitiza,
katika matukio hayo ya biblia yanaonesha wazi hali halisi na msingi katika
kuthibitisha na kuonesha juu ya utoaji wa habari za uongo kwamba, hakuna
maelezo ya kutofahamika; kinyume chake, kuamini uongo huzalisha matokeo mabaya.
Hata upotofu wa ukweli unaoonekana kidogo unaweza kuwa na athari za hatari.
Comments
Post a Comment