MAADHIMISHO YA SIKU YA 26 YA WAGONJWA DUNIANI


Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa katika Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu iliyoko Puma, Jimbo Katoliki Singida, mnamo Februali 11, 2018.

·         Maadhimisho yalitanguliwa na Misa Takatifu iliyofanyika katika Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu-Puma na kuongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda.


·         Baada ya Misa Takatifu salamu mbalimbali zilitolewa




·         Waamini wa Parokia ya Puma, wageni kutoka majimbo jirani na sehemu nyingine nchini walijumuika katika tukio hili la pekee.






·         Jengo jipya kwa ajili ya wagonjwa wan je (OPD) katika Hospitali ya Malkia wa ulimwengu lilibarikiwa katika maadhimisho haya



·         Baraka na zawadi kwa wagonjwa zilitolewa















·         Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kama ilia da yake, aligawa rozari takatifu zipatazo 700 kwa wagonjwa aliowatembelea na waamini waliohudhuria maadhimisho hayo. Daima Mkuu huyu wa Mkoa hutembea na kapu lililojaa rozari, na pale anapokutana na watu wenye uhitaji basi anawavalisha kwa upendo. (Na Pascal Mwanache)

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU