JUMAPILI YA 4 YA KWARESIMA SIKU YA KUCHANGIA JUBILEI YA MIAKA 150 YA UINJILISHAJI
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu
Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Euzebius Nzigilwa amesema kuwa hayo ni maazimiao
ya Mkutano wa TEC wa Januari 25 mwaka
huu .
Kauli mbiu ya Jubilei hiyo ni
‘Miaka 150 ya Uinjilishaji, Furaha ya Injili.’
“Machi 11 mwaka huu yaani
Jumapili ya 4 ya kwaresima (Laetare) hakutakuwa na michango mingine yoyote ya
kiparokia siku hiyo. Sadaka yote ya kwanza na ya pili ikusanywe na kupelekwa
Jimboni ili iweze kuwasilishwa Taifani.
Pia jumapili hiyo itumike kwa
ajili ya kuhamasisha waamini juu ya
maadhimisho ya Jubilei hiyo ambayo kilele chake ni Oktoba 7 mwaka huu huko
Bagamoyo badala ya Oktoba 2 mwaka huu kama ilivyokuwa imetangazwa awali,”
ameeleza Askofu Nzigilwa.
Aidha ameeleza kuwa, Mapadri,
Watawa na Waamini wote wanaalikwa kujiandaa na kushiriki kwa ibada na hija; na
kwa hali na mali katika maadhimisho ya Jubilei hiyo katika ngazi ya Parokia,
Jimbo, Kanda (Metropolitan) na Kitaifa.
Aidha, Makundi mbalimbali ya
Familia ya Mungu yanatakiwa kufanya maadhimisho ya Jubilei hiyo katika ngazi ya
Jimbo katika muda tofauti.
Vijana wanapaswa kufanya maadhimisho yao Machi 25 mwaka huu, watawa
April 8 mwaka huu, Wazee April 15 mwaka huu na Walei Mei 20 mwaka huu.
Aidha watoto wanapaswa kufanya
maadhimisho yao Juni 3 mwaka huu, Jumuiya ndogondogo Julai 8 mwaka huu, Vyama
vya Kitume Agosti 12 maka huu na Mapadri Septemba 2 mwaka huu ndipo makundi
hayo yote yataungana kwenye kilele Oktoba 7 mwaka huu Bagamoyo.
Tarehe za maadhimisho hayo ya
makundi ni kwa nchi nzima.
Waamini wanahimizwa kusali Sala Maalum ya
Jubilei katika parokia, jumuiya na katika vyama vyao vya kitume.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki
Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesisitiza waamini wa Jimbo
Kuu Katoliki Dar es Salaam kushiriki
vema na kufanya utekelezaji wa maagizo hayo ili kufanikisha jubilee hiyo.
Amewaasa hasa wale walengwa wa
kufanya maadhimisho ya makundi maalumu, walezi na viongozi wao wamuone mapema
iwezekanavyo kueleza namna watakavyoshiriki pamoja na mapendekezo ya mahali
yatakapofanyika maadhimisho hayo.
Kamati Kuu ya maandaliazi ya
Jubilei hiyo kitaifa imewasihi maparoko kuhimiza waamini wao juu ya Jubilei
hiyo na kushiriki kwa wingi katika maadhimisho ya makundi na maadhimisho ya
kilele huko Bagamoyo Oktoba 7 mwaka huu.
Comments
Post a Comment