UTOAJI MIMBA, VIDHIBITI MIMBA TISHIO NCHINI
n Na Pascal Mwanache, Dar
IMEELEZWA
kuwa utoaji wa mimba na matumizi ya vidhibiti mimba ni dhana zinazolenga
kuharibu taifa na kushambulia maadili, utamaduni na imani ya taifa huku dhana
hizo zikiwa ni itikadi ovu za magharibi za kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Uhai nchini (Pro life) Emil
Hagamu katika tathmini yake ambapo amesema kuwa utoaji wa mimba na matumizi ya
vidhibiti mimba ni vitu vigeni kwa waafrika na ili vikubalike hutumika kampeni
na propaganda yenye maneno mazuri ili kuficha uovu uliomo ndani yake.
“Taifa
lolote linaweza kuangamizwa njia ya vita. Vita kubwa tunayopigwa watanzania ni
mashambulizi dhidi ya maadili ya Taifa ambayo ndiyo yanayotafsiri jamii ilivyo.
Ukiua utamaduni unaojenga misingi ya maadili na imani utakua umeua taifa. Na
ukitaka kuua vizuri Taifa basi lenga kwa vijana, ukibomoa misingi ya hawa
lazima utamomonyoa taifa”
Aidha
amesema kuwa fikra za kuzaa, idadi ya watoto, na namna ya kupishana kwa watoto
ni sehemu ya mila na desturi za watu husika, ambapo tangu mwanzo mwanadamu
amekuwa na uelekeo wa kupenda kuzaa watoto wengi.
Ameongeza
kuwa Afrika inaongoza kwa kuwa na desturi ya kupenda na kuthamini uhai wa
mwanadamu ndiyo maana watoto ni kitu cha thamani sana katika jamii zao.
“Watu
wa Ulaya wamepita katika miongo mbalimbali, imefikia mahali wameharibikiwa. Hivyo
mawazo na itikadi zao ovu ndizo zinazoletwa kwetu Afrika hasa Tanzania.
Wanaleta kampeni za kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu kwa kuweka matumizi ya
vidhibiti mimba na utoaji mimba. Wanatumia maneno mazuri kama afya ya uzazi,
yaani wanaangalia uzazi kama kitu kinachoharibu afya” amesisitiza.
Amesema
kuwa ni uongo mkubwa kusema uzazi wa mpango unapunguza mimba zisizotarajiwa, na
kusema kuwa uzazi wa mpango unachochea mimba zisizotarajiwa, akitolea mfano wa
nchi ya Marekani ambako kuna kiwango cha udhibiti mimba kwa asilimia 80 lakini
bado kuna sheria za utoaji mimba zimetungwa.
“Wanasema
vidhibiti mimba vinasaidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto, hii siyo
kweli. Kinachosaidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto ni mipango mizuri,
utashi wa kisiasa na huduma bora za afya. Ni kuelimisha wahudumu, kuwa na vifaa
vya kutosha na wataalamu, kutoa huduma kwa uzalendo ili mhudumiwa aone kuwa
sehemu ya huduma ni sehemu salama na siyo sehemu ya kifo” ameongeza.
Ameeleza
kuwa dawa zinazotumika kudhibiti mimba zinageuza uzazi kuwa ugonjwa na mtoto
anayepatikana na uzazi kuwa balaa, huku akitahadharisha kuwa kiwango cha
wanawake wanaoshindwa kupata mimba kinaongezeka ikiwa ni madhara ya matumizi ya
dawa hizo.
Pia
amesema hiyo inaashiria kuwa kwa sasa uwezekano wa wasichana kuolewa ni mdogo
kuliko ilivyokuwa zamani, na kubainisha kuwa asilimia 25 ya wasichana
wanaotumia vidhibiti mimba chini ya umri wa miaka 25 wanapata saratani ya
matiti.
Katika
hatua nyingine Ndugu Hagamu ametahadharisha kuwa kuna sera zinazotekelezwa na
serikali na washirika wengine juu ya afya ya uzazi ambazo zinaweza kuliangamiza
taifa, kwani walengwa wa sera hizo ni vijana kuanzia miaka 15, ambapo amesema
kuwa umri huo siyo sahihi kuwachanganyia mitaala ya mahusiano.
“Mtoto
hastahili kuzaa wala kupanga uzazi kwani kwa umri huu anastahili kuwa shuleni.
Huu ni umri wa makuzi na malezi na kwa kuwa hajafikisha miaka 18 anakuwa yupo
chini ya uangalizi wa wazazi. Sasa inastaajabisha, eti watoto wa miaka 15
wanawekwa kwenye kampeni za kuwafundisha afya ya uzazi ikiwa ni pamoja na haki
ya kuwa huru katika kufanya maamuzi ya mahusiano na jinsia. Wanafundishwa
shuleni na vyuoni mambo haya, na wanayaita afya ya uzazi kwa vijana. Hili taifa
linakwenda wapi?” amehoji.
Ameeleza kuwa dawa zinazotumika kudhibiti mimba zinageuza uzazi https://digg.com/u/tuvanphathai kwani walengwa wa sera hizo ni vijana kuanzia miaka 15, ambapo amesema kuwa umri huo siyo sahihi kuwachanganyia mitaala
ReplyDelete