2124 kuhitimu SAUT
WAKATI
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) Mwanza kikijiandaa na
mahafali ya 19 yatakayofanyika Desemba 8 na 9, 2017, takribani wanafunzi 2124
sawa na asilimia 79 wanatarajia kuhitimu masomo yao huku wanafunzi 424
wakishindwa kuhitimu elimu yao ya chuo kutokana na sababu mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari chuoni
hapo Makamu Mkuu wa SAUT Padri Dkt. Thaddeus Mkamwa amebainisha kuwa takribani
wanafunzi 424 sawa na asilimia 21 ya jumla ya idadi ya watakaohitimu mwaka huu watashindwa
kupata vyeti vyao vya ngazi ya cheti stashahada na shahada
Padri Mkamwa amebainisha kuwa wanafunzi wengi wameshindwa
kuhitimu kwa sababu ya uzembe wa kitaaluma, wengine kushindwa kulipia gharama
za masomo na pia baadhi matatizo ya kiafya
Kuhusu wanafunzi walioshindwa kuhitimu kwa sababu ya
kitaaluma, Padri Mkamwa amesema kuwa wengi wao walishindwa katika masomo yao na
wengine kushindwa kumaliza masomo yao ya utafiti ambayo kama mwanafunzi wa SAUT
hutakiwa kufanya utafiti.
Pia maandalizi hayo ya mahafali hutanguliwa na siku ya
kijamii ya SAUT ambapo wanafunzi na wahadhiri wao huitumia kwa ajili ya
maonesho ya kitaaluma ambapo pia Makamu Mkuu wa chuo amewaomba wanafunzi ambao
wameshindwa kudahiliwa chuoni hapo na pia kushindwa kupata pesa zao za mkopo,
chuo kimezungungumza na benki ya CRDB na kukubaliana nao na wanafunzi
wanatakiwa kuwasiliana na binki hiyo kwa utaratibu waliojiwekea
Mahafali ya 19 ya SAUT yatafanyika katika viwanja vya Rila
Odinga na yataanza na adhimisho la misa takatifu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu Yuda Thaddeus
Ruwa’ichi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya wamiliki wa Vyuo, huku Mkuu wa
Chuo hicho atawakilishwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Flavian
Kasalla na Askofu wa Jimbo Katoliki Mbinga Mhashamu John Ndimbo.
Comments
Post a Comment