WAKATOLIKI NA WALUTERI KAMWE WASIWE MAADUI-PAPA FRANSISKO
Baba Mtakatifu amekutana na wajumbe wa Shirikisho la Kiluteri duniani mjini Vatican walioongozwa na Askofu Mkuu wa Nigeria Musa Panti Filibus ambapo ametoa salam na pongezi kwa Dk. Junge, Katibu Mkuu na Mwenyekiti Msaidizi na wajumbe wa Shirikisho la Kiluteri Duniani, kwa hotuba na kumpongeza kuchaguliwa kwake hivi karibuni.
Hotuba hiyo akielekeza kwa Askofu Mkuu Musa anasema, kwa pamoja wanaweza kufanya kumbukumbu kama maandiko matakatifu yanavyofundisha kuwa Mungu ametutendea makuu! (Zab 77,12-13). Baba Mtakatifu anasema, kumbukumbu ni kwa namna ya pekee katika vipindi vyote vya mikutano ya kiekumene vilivyofanyika katika kipindi chote cha mwaka wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mageuzi ambayo imehitimishwa siku chache zilizopita. Aidha anaongeza kusema, anapenda kukumbuka hasa tarehe 31 Oktoba 2016 waliposali pamoja huko Lund Sweden, mahali lilipoanzishwa Shirikisho la Kiluteri duniani.
Ilikuwa ni jambo muhimu kukutana, hasa katika salamu na hili si katika mipango ya kibinadamu, bali kwa neema ya Mungu, vichipukizi viweze kutoa zawadi ya umoja kati ya waamini. Na hivyo ni kwa njia ya sala tu, inawezekana kulinda mmoja na mwingine. Sala inatakasa,inatoa nguvu,inaangaza njia na kufanya kwenda mbele. Sala ni kama petroli ya katika safari ili kuelekea umoja wa kweli.
Hiyo inajidhihirisha katika upendo wa Bwana utokanao na kusali, umoja unajikita katika nguvu ya upendo ambao unatufanya kukaribiana, kuwa na uvumilivu kutokana na mabadiliko ya uongofu na nguvu ya kwenda mbele pamoja. Ni kuanzia katika sala ndipo inawezekana kuwa na roho ya mabadiliko ya kiekumene na vishirio vya umoja, pia mazungumzo yanajengwa na kuonekana katika msingi wake.
Aidha akitafakari juu ya sala anasema, ni kutazama juu ya historia iliyopita na kumshukuru Mungu, kwasababu mgawanyiko japokuwa ulileta uchungu ambao ulisababisha kuwa mbali kwa mihongo mingi, kwa bahati katika miaka ya mwisho imeonesha hatua nyeti ya safari ya kuelekea katika umoja ambayo ni safari ya kiekuemene, inayotokana na nguvu ya Roho Mtakatifu. Njia hiyo imetufanya kuachilia mbali vizingiti vilivyojitokeza kipindi cha Martin Luteri na juu ya hali halisi ya Kanisa Katoliki katika kipindi hicho.
Safari ya kiekumene imechangia kwa kiasi kikubwa mazungumzo katika Shirikisho la Kiluteri Duniani na Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha umoja wa Wakristo, ulioanzishwa tangu mwaka 1967. Mazungumzo ambayo yanafanya kumbukumbu ya shukrani leo hii kwa miaka 50 iliyopita; ni kutambua baadhi ya maandiko muhimu ambayo ni Mkataba wa pamoja juu ya Mafundisho ya haki na Waraka kutoka kipindi cha migogoro kufikia umoja.
Katika kumbukumbu ya utakaso leo hii, tunaweza kutazama kwa imani wakati ujao ambao hauna migongano tena na mantiki zilizopita. Ni wakati ambao utajikita katika upendo wa pamoja (Rm,13,8). Ni wakati ambao wote tunaalikwa kuchagua zawadi zitokazo kwa kila tamaduni tofauti za kidini na kupokea na kukubali kama urithi wa pamoja. Kabla ya mvutano,utofauti na majeraha yaliyopita, Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa ipo hali halisi ya wakati uliopo yaani ya umoja unajikita katika msingi wa kudumu wa ubatizo wetu.
Ubatizo umetufanya sisi sote kuwa wana wa Mungu na ndugu kati yetu. Na kwa njia hiyo haiwezekani tena kuruhusu uadui uingilie kati. Iwapo wakati uliopita hauwezekani kuubadili, basi wakati ujao unatualika, kuwa haiwezekani kurudi nyumba, na hivyo sasa ni kutafuta kuhamasisha kwa nguvu umoja na katika upendo na imani.
Tunaalikwa pia kukesha mbele ya majaribu yanayojitokeza katika safari yetu ndefu. Katika maisha ya kiroho kama yale maisha ya Kanisa, iwapo unasimama ni kurudi nyuma , kwasababu ya kuridhika, kuwa na hofu, uvivu, uchovu au mambo mengine yanayojitokeza wakati wa safari kuelekea kwa Bwana na ndugu zake. Baba Mtakatifu anawaalika kujikita zaidi katika kujibu, hasa kutazama maskini na ndugu wadogo wa Bwana (Mt 25,40).
Hizo ndizo ishara msingi katika safari yetu tunazohimizwa, na itakuwa vizuri zaidi kugusa majeraha kwa nguvu ya uponyaji, katika uwepo wa Yesu kwa njia ya dawa ambayo ni huduma yetu. Na ili iweze kutimilizika kuwa na umoja, ndiyo safari ambayo tunaitwa kwa jina la Yesu. Lakini bado kuna siku nyingi za kuteseka kwasababu ya kutoa ushuhuda wa Yesu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Comments
Post a Comment