UJUMBE WA PAPA FRANSISKO KWA SIKU YA 26 YA WAGONJWA DUNIANI 2018
“TAZAMA
huyo ndiye mwanao … tazama huyo ndiye mama yako. Na tangu saa ile huyo
mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake”(Yoh. 19:26-27), ni utangulizi wa
Ujumbe wa Papa Fransisko kwa siku ya 26 ya Wagonjwa Duniani hapo mwaka 2018,
ambapo amesema kuwa Kanisa na wahudumu wa wagonjwa wanapaswa kufanya huduma zao
kwa uaminifu wa utume wa Bwana. (Lk 9,2-6: Mt 10,1-8; Mk 6,7-13).
Kauli mbiu ya Siku ya Wagonjwa
Duniani 2018 imechaguliwa kutoka katika
maneno ya Yesu aliyotamka msalabani, akimwelekea mama yake Maria na
Yohane: Mama wa Kanisa “Tazama huyo ndiye mwanao … tazama huyo ndiye mama yako.
Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake” (Yh
19:26-27).
Katika ujumbe huo, Baba
Mtakatifu anasema, Maneno ya Kristo yanaangaza kwa kina fumbo la Msalaba.
Maneno hayo hayawakilishi janga hilo bila matumaini, bali ni mahali ambapo Yesu
anaonesha utukufu wake alijiachia kwa utashi wa upendo wake upeo.
Amesema kuwa maneno ya Yesu
yanatoa chanzo cha wito wa umama wa Maria mbele ya binadamu wote. Yeye kwa
namna ya pekee anakuwa mama wa mitume na mwanae. Anachukuwa wajibu wa kuwatunza
na katika safari yao. Wote tunatambua kuwa utunzaji wa mama kwa mwanae huanzia
katika mantiki zote ziwe katika nyenzo na hata kiroho kwa mafundisho yake.
Injili inasema, “katika uchungu
ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wa Maria” (Lk2,35) lakini haumwogopeshi.
Badala yake, kama Mama wa Bwana anaanza yeye safari moja kwa moja ya kujitoa
yeye binafsi. Akiwa msalabani, Yesu anahangaikia Kanisa na binadamu wote, na
Maria anaitwa kushirikishwa wasiwasi wa Yesu.
Baba Mtakatifu Fransisko anasema
kuwa, katika kitabu cha Matendo ya Mitume, kikielezea juu ya tukio la Roho
Mtakatifu Siku ya Pentekoste, kinaonesha kuwa Maria alianza shughuli yake
katika Jumuiya ya kwanza ya Kanisa. Ni kazi ambayo haina mwisho.
Mtume Yohane, mpendwa, anawakilisha
Kanisa, ambao ni watu kinabii. Yeye ni lazima atuambie kuwa Maria ni mama
yake. Na katika utambuzi huo, anaalikwa kupokea na kutafakri Maria kama
mfano wa utume na hata wito wa mama ambaye Yesu amemkabidhi, ikiwa ni pamoja na
wasiwasi wake na mipango yote itokanayo na wito huo; kwa maana ni mama
anaye penda na kuzaa watoto wenye uwezo wa kupenda kwa mujibu wa amri ya Yesu.
Kwa njia hiyo wito wa mama Maria
yaani wito wa kutunza watoto wake, unapitia kwa njia ya Yohane na Kanisa zima.
Na Jumuiya nzima ya mitume wanahusika katika wito wa mama Maria.
Yohane kama mtu anayeshirikishwa
na Yesu kila kitu anatambua jinsi gani Mwalimu wake anataka kuwakusanya watu
wote wakutane na Baba.Yeye anaweza kushuhudia kuwa Yesu alikutana na watu
wengi wakiwa wagonjwa wa kiroho na kwa sababu
wamejaa kiburi (Yh 8,31-39) pia wagonjwa kimwili (Yh 5,6). Na kwa watu wote
aliwapa huruma na msamaha.
Na wagonjwa kimwili wakapona, na
ishara ya maisha yaliyojaa Ufalme, ni mahali ambapo machozi yanakaushwa. Kwa
njia hiyo, kama Maria, mitume wanaalikwa kuhudumiana. Pia wanatambua ya kwamba,
moyo wa Yesu huko wazi kwa wote bila ubaguzi. Wote wanapaswa kupashwa habari ya
Injili ya Ufalme, wote ambao wanahitaji, wanapaswa kuelekezwa katika upendo wa
kikristo kwa urahisi, kwa sababu ni watu, na wana wa Mungu.
Wito wa umama katika Kanisa, kwa
ajili ya wahitaji na wagonjwa umejidhihirisha katika historia ya miaka elfu
mbili iliyopita, katika utajiri wa kuanzisha mipango mingi kwa ajili ya
wagonjwa. Ni historia ya kujikita katika shughuli hiyo bila kusahau.
Hata leo hii inaendelea katika
dunia. Baba Mtakatifu anafafanua kuwa, katika nchi ambazo kuna mipango ya Afya
ya umma inayojitosheleza, shughuli ya mashirika Katoliki, katika majimbo na
mahospitali, zaidi ya kutoa tiba za hali ya juu pia wanatafuta kwanza
kumweka binadamu awe ni kitovu katika mchakato wa tiba na kuendelea na
utafiti wa kisayansi kulingana na maisha na thamani zake za kimaadili ya
kikristo.
Katika nchi ambazo kuna uhaba wa
mipango ya afya, au kutokuwapo kabisa, Kanisa linajikita kutoa kile ambacho
inawezekana kwa watu, kama vile utunzaji na afya, ili kuondoa na kupunguza vifo
vya watoto wachanga. Aidha hata kuwasaidia baadhi ya wengine wenye magojwa ya
kuambukiza.
Kila mahali Kanisa linajitahidi
kutibu, hata kama halina uwezo wa kuponyesha. Sura ya Kanisa “kama hospitali
iliyoko katika kambi”, inapokea wote waliojeruhiwa katika maisha. Ni hali
halisi na ya dhati kwa sababu katika maeneo mengi ya ulimwengu, zipo hospitali
za wamisionari na katika majimbo ambayo wanatoa huduma ya tiba muhimu kwa watu.
Kumbukumbu ndefu ya kihistoria
ya huduma kwa wagonjwa; ni sababu ya furaha kwa jumuiya ya kikristo na kwa
namna ya pekee kwa wale wanaotoa huduma hiyo nyakati za sasa. Baba Mtakatifu
anafafanua kuwa ili kuweza kufanya hivyo, ni lazima kutazama yaliyopita ili
kujitajirisha kutokana nayo.
Yote hayo ni lazima kujifunza
kutokana na ukarimu hadi kujitoa sadaka ya moja kwa moja kwa waanzilishi wengi
wa mashirika ya huduma ya wagonjwa kama vile ubunifu unaoelekezwa kutokana na
upendo, shughuli nyingi zilizoanzishwa katika miongo mingi, shughuli za utafiti
kisayansi, ili kuweza kutoa tiba kwa wangojwa kwa njia ya ubunifu na matibabu
ya kuaminika.
Anathibitisha zaidi kwamba,
urithi huo wa kizamani unasaidia kupanga vizuri mipango ya baadaye.
Kwa Maria, Mama wa huruma,
tunataka kumtolea wagonjwa wote, ikiwa ni kimwili na kiroho, ili awaweke katika
tumaini. Kwake yeye tunamwomba pia kutusaidia tuwe wakarimu kwa kuwapokea ndugu
wagonjwa. Kanisa linatambua kuwa na haja ya neema malumu ili kuweza kujikita
katika huduma yake kiinjili kwa ajili ya wagonjwa. Kwa njia ya sala kwa mama wa
Bwana, atutazame wote tunaounganika katika maombi ili kila mwanachama wa Kanisa
awe hai na upendo wa wito wa huduma ya maisha na Afya.
Baba Mtakatifu anamalizia ujumbe
wake akisema, Bikira Maria aombee siku ya 26 ya Wagonjwa duniani, asaidie
wagonjwa wote waishi katika mateso yao na muungano na Bwana Yesu; awasaidie
hata ambao wanawasaidia katika matibabu. Na kwa wote: wagonjwa, wahudumu wa
Afya, watu wa kujitolea, anawapa Baraka yake.
Vatikani Novemba 26, 2017
Sikukuu ya Bwana wetu Kristo Mfalme wa Ulimwengu
Sikukuu ya Bwana wetu Kristo Mfalme wa Ulimwengu
Comments
Post a Comment