PAPA:MARIA ATUSAIDIE KUONGEZA KINGA ZA KIMWILI DHIDI YA VIRUSI VYA NYAKATI ZETU


Kama utamaduni, hata mwaka huu Baba Mtakatifu jioni ya tarehe 8 Desemba 2017 amekwenda uwanja wa Hispania, ili kutoa heshima chini ya Miguu ya Sanamu ya Bikira Maria katika Sikukuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili. Sikukuu hiyo ni kulingana na Waraka wa mafundisho ya Papa Pio IX  yaliyotolewa tangu tarehe 8 Desemba 1854.
Katika sala ya Baba Mtakatifu Fransisko kwa mama Maria, ameomba na ulinzi wake kwa jina la wakazi wa Roma. Ni sala ya moja kwa moja ya kina, akimshukuru Mama Maria Mkingiwa dhambi  ya asili jinsi anavyozidi kulinda na kutusindikiza katika safari yetu. Kwa ajili ya familia, parokia, na  jumuiya mbalimbali za kidini, hata kwa wote  shida kubwa ya kusafiri kila siku mjini Roma kwenda kazini. Kwa ajili ya wagonjwa, wazee, na maskini wote na pia wahamiaji wanaotoka katika nchi za vita na njaa.
Baba Mtakatifu amekumbuka wote bila kumsahau hata mmoja wakati wa kutoa shukrani kwa Mama Maria katika uwepo wake wa kimama, ukarimu na nguvu. Anaomba asaidie Mji wa Roma ili uweze kuongeza kinga za mwili, dhidi virusi vya nyakati zetu za sintofahamu na utofauti, tabia mbaya kimaadili, ambayo inadharau wema wa pamoja, aidha hofu ya kuogopa aliye fotauti na mgeni. Ameomba kuondokana na kulinganisha au unafiki, uchafuzi wa mazingira na maadili. Katika hilo anaongeza kuomba juu ya tabia za  unyanyasaji na unyonyaji wa watu wengi wake kwa waume.
Baba Mtakatifu ametoa ombi kwa Mama Maria ili  watu wote waweze kusoma kila siku Injili ili kwa njia ya mfano wake, tujifunze sote kutunza Neno la Mungu na kuliweka katika matendo. Akikumbukwa uongofu wa Alfonso Ratisbonne uliotokea katika Kanisa la Mtakatifu Andrea Fratte Roma, hatua chache kutoka kiwanja cha Hispania, mahali ambapo Maria alijionesha kama “Mama wa neema na huruma”; Baba Mtakatifu amemwomba Maria ili sote  hasa wakati wa majaribu ya vishawishi, si kutazama uso wake tu bali ha kujivua kila aina ya maneno mabaya, ili kuweza kutambua kuwa sisi kweli ni wadogo na maskini wadhambi  lakini daima ni watoto wake.
Sala yake imehitimisha akiomba tushikwe mkono tupelekwe kwa Mungu na Mama Maria mkingiwa wa dhambi ya asili, kwa maana, Baba wa mbinguni hachoki kusubiri na kusamehe wale wanaotaka kurudi kwake.
Baada ya sala na heshima ya kuweka maua chini ya miguu ya Sanamu ya Bikira Maria, Baba Mtakatifu Fransisko, amesalimia watu na kuwabariki hasa idadi kubwa ya wagonjwa waliosindikizwa na watu wa kujitolea katoka Kitengo Unitalsi cha Roma na wengine kutoka  Mkoa mzima wa  Lazio Italia.
Habari mpya ya mwaka huu ni kwamba mara baada ya sherehe hizo. Baba Mtakatifu ametembea kwa miguu hadi katika Kanisa la Mtakatifu Andrea Fratte, mahali ambapo miaka 175 iliyopita, Alfonso Ratisbonne, asiyeamini Mungu  na adui wa wakristo alipata uongofu mbele ya picha ya Maria ambayo bado imahifadhiwa vizuri. Hata hivyo tendo la ibada hiyo imefanyika kwa namna ya faragha, kama vile alivyofanya katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kabla ya kufika katika Uwanja wa Hispania.
Historia yake:
Ilikuwa tarehe 20 Januari 1842 kijana Ratibonee aliyekuwa na shahada ya sheria na kazi ya benki lakini akiwa anajidhihirisha kumkana Mungu na adui wa wakristo. Aliingia katika Kanisa la Mtakatifu Andrea kwa utukutu tu, na kumbe akamtokea Maria, kama inavyoonesha Katika Medali ya Miujiza ya Mtakatifu Caterina wa Labouré
Katika maandishi ya Alphonse yanasema kuwa: Bikira Maria hakutamka neno, lakini nilitambua kwa uhakika…pazia ilishuka machoni pangu na kuondokana na giza nene, niliona giza la kina hasa la dhambi nilizokuwa nazo kwa njia ya huruma isiyokuwa na kikomo.
Baada ya kuona tukio hilo, aliomba kubatizwa, na baadaye akawa kuhani. Na tangu wakati huo, Kanisa la Mtakatifu Andrea likawa mahali pa ibada ya Maria. Katika Kanisa hilo. Kikanisa cha tatu kushoto Picha ya Mama maria wa miujiza inapatikana, vilevile kama ilivyomtokea Kijana Ratibonne.
Kutokana na uongofu wa watu wengi, Papa Benedikto XV alielezea kuwa ni madhabahu ya Maria  wa Lourdes Waroma, ambapo hata leo hii upo uwezekano wa maondoleo ya dhambi kwa mujibu wa hali zake.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI