Papa Francisko kutembelea S. Giovanni Rotondo 17 Machi 2018

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 tangu alipofariki dunia Mtakatifu Padre Pio wa Pietrelcina, tarehe 17 Machi 2018 anatarajiwa kufanya hija ya kichungaji mjini Pietrelcina, Jimbo Katoliki la Benevento, Italia. Maadhimisho haya yanakwenda sanjari na Jubilei ya Miaka 50 tangu Madonda Matakatifu yalipojitokeza kwenye mwili wa Padre Pio alipokuwa katika huduma huko San Giovanni Rotondo, Jimbo Katoliki la Manfredonia-Vieste. Haya yamebainishwa na Dr. Greg Burke, Msemaji mkuu wa Vatican, Jumanne, tarehe 19 Desemba 2017
Itakumbukwa kwamba, Mtakatifu Padre Pio alizaliwa kunako tarehe 25 Mei 1887 huko Pietrelcina, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi na Kitawa, alipadrishwa kunako tarehe 10 Agosti 1910 na kufariki dunia kunako tarehe 23 Septemba 1968 huko San Giovanni Rotondo. Alitangazwa kuwa Mtakatifu na Papa Yohane Paulo II kunako tarehe 16 Juni 2002 na Mama Kanisa anafanya kumbu kumbu yake kila mwaka ifikapo tarehe 23 Septemba.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Vatican News.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI