"BARAZA LIMEPOTEZA KIUNGO KIKUBWA"PADRI RAYMOND SABA

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Padri Raymond Saba(pichani) amesema Baraza limesikitishwa sana na kifo cha Baba Askofu Mstaafu Mhashamu Mathias Joseph Issuja aliyefariki usiku wa kuamkia leo.

Amesema marehemu ni moja kati ya viongozi waliojitolea kwa hali na mali katika kulisaidia baraza la maaskofu ili kuweza kujiendesha lenyewe pasipo kutegemea msaada.

Amesema marehemu alikuwa na msimamo sana katika kile alichokiamini,jambo ambalo limesaidia sana katika kuliletea mafanikio makubwa baraza la maaskofu katoliki.

Katibu Mkuu amewataka watumishi katika idara mbalimbali zilizopo chini ya baraza hilo kumwombea marehemu huku wakiyaishi yote aliyoyafanya katika kuliletea maendeleo baraza ikiwa ni pamoja na utendaji makini na kujitolea.

Mhashamu Mathias Joseph Issuja atapumzishwa rasmi tarehe 20 Aprili huko Dodoma kwenye kanisa kuu la Mt.Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma.

Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi AMINA.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU